Kesi zote za Uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika Machi 2016

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Jaji Kiongozi Shaban Ali Lila aaagiza kesi zote za pingamizi zinazohusu uchaguzi kuharakishwa na kumalizika mwezi Machi 2016.

=========================

Dodoma. Majaji na mahakimu kote nchini wameagizwa kumaliza kesi zote zinazohusiana na masuala ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, ifikapo mwishoni mwa Machi 2016 na.
Jaji+Kiongozi+PHOTO.jpg

Jaji Kiongozi, Shaban Ali Lila

Agizo hilo lilitolewa jana na Jaji Kiongozi, Shaban Ali Lila wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mahakimu wakazi wa mikoa na wilaya ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo hayo kwa nchi nzima ili kuwajengea uwezo watumishi hao katika kumaliza kwa wakati, kesi za kupinga ushindi kwa waliochaguliwa.

Huo ni mwendelezo wa mafunzo yenye lengo la kumaliza mapema kesi zinazotokana na uchaguzi ili kuondoa manung'uniko.

Tayari kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi kwa ngazi ya ubunge zimeshafunguliwa katika sehemu mbalimbali nchini.

Katiba ya Tanzania inaruhusu kupinga mahakamani, matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani lakini hairuhusu kupinga matokeo ya urais.

Jaji Lila alisema sheria inaeleza kuwa kesi za uchaguzi zimalizwe na kutolewa hukumu ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

"Tunatakiwa kujenga imani kwa chombo chetu kwani ndiyo sehemu ya kimbilio la watu kutafuta haki yao, tutumie walau miezi mitano na ndiyo maana nikasema hadi mwisho wa Machi mwakani (2016), tusiwe na kesi inayohusu uchaguzi," alisema.

Aliagiza kesi hizo kupewa kipaumbele cha kwanza na ziamuliwe kwa kufuata weledi wa mahakimu huku akitaka watende haki bila ya kumuonea mtu aibu ili wajipambanue kwa weledi wao.

Hata hivyo, mahakimu walionyesha shaka ya kutimiza lengo hilo wakisema siyo wanaokwamisha kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Manyara, Devotha Kamuzora alisema wanaochelewesha kesi siyo mahakimu, bali ni mawakili wa walalamikaji au walalamikiwa.

Alisema mawakili mara nyingi wanakuwa na kesi nyingi za kutetea watu katika mahakama tofauti na wakati mwingine mikoa tofauti jambo linalowafanya kuwa na visingizio vingi.

Mwakilishi wa UNDP inayoratibu mafunzo hayo, Clement Gba, aliwataka mahakimu kutenda haki kwa watu wote maskini na matajiri bila ya kuangalia kama wanatoka vijijini au mijini kwani haki inasimama kwa mtu yeyote.

Chanzo: Mwananchi
 
Wao wana mehela ya kumwaga kwa ajili ya kesi za uchaguzi, hivyo macho yao ni jinsi ya kuzitafuna fasta.
 
Yaani hili jambo ni gumu na halitekelezeki
kama mnabisha ngoja Moderators wauweke uzi huu
uwe sticky hapa mpka hiyo machi, kisha tuje kuona kama
hata 40% ya kesi zote zitakuwa zime siklizwa.

Danganya toto hiyo.
 
Yaani hili jambo ni gumu na halitekelezeki
kama mnabisha ngoja Moderators wauweke uzi huu
uwe sticky hapa mpka hiyo machi, kisha tuje kuona kama
hata 40% ya kesi zote zitakuwa zime siklizwa.

Danganya toto hiyo.

Ni vigumu kesi kwisha ndani ya miezi 6 hasa ukiwa na wakili kama tundu lissu,mara arudi bungeni mara utaambiwa kaenda mwanza kuwatoa bavicha kituo cha polisi.
 
Back
Top Bottom