Kesi za kuzuia uchaguzi TLS zatupiliwa mbali na Mahakama Kuu, uchaguzi uko pale pale

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Ile kesi ya kupinga uchaguzi wa TLS iliyofunguliwa Dar es Salaam na Dodoma zimetupiliwa mbali.

Kesi moja ilifunguliwa Mahakama Kuu, Dar es Salaam na wakili Onesmo Mpinzile. Wakili Masha na wenzie 'amewahenyesha' waliofungua kesi hiyo na leo rasmi jaji kaitupilia mbali.

Kesi ya Dodoma ilifunguliwa na wakili Wasonga, Wasonga alipigwa mapingamizi kumi na tano ya kisheria na kikosi cha wanasheria visiki wakiongozwa na Lissu nayo imetupiliwa mbali.

Mahakama imewataka Mawakili Onesmo Mpinzile na Godfrey Wasonga kulipa gharama za kesi.

 
Ile kesi ya kupinga uchaguzi wa TLS iliyofunguliwa DSM imetupiliwa mbali.

Kikosi kazi cha lissu na wenzie kimewahenyesha waliofungua kesi hiyo mpaka wakaishiwa pumzi na leo rasmi jaji kalifuta kesi hilo.


Imebaki kesi ya Dodoma ambayo wakili wasonga alipigwa mapingamizi kumi na tano ya kisheria na kikosi cha wanasheria visiki wakiongozwa na lissu

Wakili wasonga alitaka kuiondoa kesi hiyo baada ya kuona "misumari" ya kisheria ya akina lissu lakini akina lissu waligoma,wakataka wasikilizwe ili wamchape kweli kweli,hakika walimchapa wakili huyo wa ccm na maamuzi ni Leo

Mapingamizi hayo yaliibomoa kesi hiyo na kila kitu kilitupwa na ilibaki paragraph moja tu ,jina la mahakama na mleta maombi
si mmesema amekamatwa na yuko kwenye defender anarudishwa dar kukabiliwa na kesi ya kuruka dhamana?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom