Kesi za Kupinga matokeo ya Ubunge.

vivian

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,749
1,000
Ni wazi kwamba Serikali hii ya Awamu ya Nne imekua na kesi nyingi za kupinga matokeo ya Ubunge kuliko serikali ya awamu yeyote ile katika Historia ya nchi yetu.

Kwa vile hapa jamvini kuna makada wa vyama tofauti, Tunashangalia pale Mbunge wa upande wetu ameshinda kesi au pale mbunge wa chama Pinzani amevuliwa ubunge.

Hapa naona tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe,
Gharama za uchaguzi ziko juu sana, kurudia uchaguzi ni kujiingiza katika gharama ambazo tungeweza kuziepuka kama mamlaka husika zingeweza kusimamia vyema swala zima la Uchaguzi.

Mpaka sasa kuna wabunge wawili wamevuliwa Ubunge, Mmoja wa Chadema na mwingine wa CCM. Kwahiyo mpaka dakika hii ni ngoma Droo kwa vyama vyote.

Who do you think is in the loosing End up to this point?
 
Nadhani mwaka 1995 vyama vya nccr na ccm vilipinga matokeo ya chaguzi nyingi, idadi inayoweza kulingana na wakati huu.
Kuhusu mada uliyoileta, nashauri pale inapothibitika kwamba usimamizi wa uchaguzi ulikuwa na makosa basi wasimamizi waliosababisha makosa hayo walipe fidia ili iwe fundisho na kuongeza umakini. Na inapothibitishwa kwamba mgombea alikiuka taratibu, basi yeye ndiye alipe gharama zote ikiwemo kurudia uchaguzi. Mfano aliyekuwa mbunge wa sumbawanga (ccm) amethibitika kufanya vitendo vya rushwa. Huyu anatakiwa kulipia gharama za kesi na kurudia uchaguzi pamoja na kuhukumiwa kwa kosa la rushwa maana limethibitika mahakamani.
Sikubaliani na swala la kukwepa kurudia uchaguzi kwa kisingizio cha gharama maana wananchi wanaweza kulazimishiwa mbunge ambaye hawakumchagua na kusababisha kutotoa ushirikiano kwake jambo litakalorudisha nyumba maendeleo. Angalia Igunga mbunge anavyozomewa kila akirudi jimboni. Tatizo ni kwamba hawakumchagua lakini wakalazimishiwa!
 
Demokrasia ina garama hata hivyo badili title yako watu tutoe maoni sawa na unachokusudia kupata, usitumie jila la jimbo au mbunge wa cdm ili kuvuta watu kwenye hii thread, utapata visitor wengi kuliko wachangiaji.
 
Demokrasia ina gharama kubwa sana kuliko gharama za uchaguzi hata siku moja usijaribu ku compromise demokrasia na gharama! Je waonaje mtu akauibia mali zako wewe ukaenda mahakamani mahakama ikasema kundesha kesi yako ni gharama sana hivo mwache tu huyu mwizi???Hali kadhalika wapiga kura wametoa sauti yako lakini mtu au tume ya uchaguzi wakavuruga matokea na kumtangaza ambaye sio sauti ya wapiga je kwa sababu ya kuogopa gharama basi tuache tu hawa wezi wa kura na wachakachuaji waendelee na matendo yao maovu??nini sasa maana ya utawala wa sheria??
 
Ni kweli gharama za uchaguzi ni kubwa, na hata hivyo nadhani wanaopaswa kuwajibika kwa hilo moja kwa moja ni tume ya uchaguzi kwani wao ndio chanzo cha uozo huo,
 
Hivi hata kama kusingekuwa na gharama wewe unanufaika vipi na keki ya Taifa? au wewe ni miongoni mwa walaji unaona uchungu tunazipunguza pesa zenu za kutafuna?
 
Vivian hii ndo ghalama ya demokrasia.
Lazima tupate mgombea aliye patikana kwa HAKI na si kwa ujanja ujanja na vimbinu mbinu.
 
Mkuu jaribu kutafuta munzani sahihi wa kupima kati ya DEMOKRASI na UCHAGUZI,utapata jibu.lakini nikuulize tu kunagharama kushinda uhai wa mtu(damu kumwagika?).ninavyofahamu uchaguzi gharama ni pesa tu kitu ambacho sioni kama ni hatari kama kitatumika kwa manufaa ya wananchi kuliko kama sasa zinavyoliwa na mawaziri.lakini kwa upande mwingine ni demokrasia ndio inagharama kubwa kwani kunawatu hupoteza maisha then wengine wanao bakia hunufaika.Hata mimi leo natamani kufa nikiwa natafuta/nadai haki
 
Demokrasia ni gharama kweli ila mimi nadhani mtu anayefungua kesi kama alikuwa mgombea na akashinda kesi basi atangazwe Mbunge wa jimbo husika bila kurudia uchaguzi
 
Ni wazi kwamba Serikali hii ya Awamu ya Nne imekua na kesi nyingi za kupinga matokeo ya Ubunge kuliko serikali ya awamu yeyote ile katika Historia ya nchi yetu.

Kwa vile hapa jamvini kuna makada wa vyama tofauti, Tunashangalia pale Mbunge wa upande wetu ameshinda kesi au pale mbunge wa chama Pinzani amevuliwa ubunge.

Hapa naona tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe,
Gharama za uchaguzi ziko juu sana, kurudia uchaguzi ni kujiingiza katika gharama ambazo tungeweza kuziepuka kama mamlaka husika zingeweza kusimamia vyema swala zima la Uchaguzi.

Mpaka sasa kuna wabunge wawili wamevuliwa Ubunge, Mmoja wa Chadema na mwingine wa CCM. Kwahiyo mpaka dakika hii ni ngoma Droo kwa vyama vyote.

Who do you think is in the loosing End up to this point?
Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia
 
ni kweli gharama ni kubwa inabidi tutafute jinsi ya kukabiliana nazo nashauri kama chama mgombea wake amehusika na kukiuka taratibu za uchaguzi chama husika kibebe gharama hii itasaidia vyama husika kuwabana wagombea wake wasikiuke maadili ya uchaguzi
 
Demokrasia ni gharama kweli ila mimi nadhani mtu anayefungua kesi kama alikuwa mgombea na akashinda kesi basi atangazwe Mbunge wa jimbo husika bila kurudia uchaguzi

mkuu hii inakua ngumu kidogo kwakua kesi hizi zinakua na madai tofauti tena si moja pengine hata madai zaidi ya moja,kuna kuiba kura,kuna matus wakti wa kampen,kuna rushwa,n.k
mi nafikiri kesi hizi ziwe zinafanyika ndani ya mwezi mmoja na kuisha il wananch wawai kupata kiongozi wanaemtaka
 
Usemayo ni kweli ila wewe unatoa wazo gani mbadala ya kurudiwa kwa uchaguzi ili aliyepiga kura aone ametendewa haki?
 
Ni wazi kwamba Serikali hii ya Awamu ya Nne imekua na kesi nyingi za kupinga matokeo ya Ubunge kuliko serikali ya awamu yeyote ile katika Historia ya nchi yetu.

Kwa vile hapa jamvini kuna makada wa vyama tofauti, Tunashangalia pale Mbunge wa upande wetu ameshinda kesi au pale mbunge wa chama Pinzani amevuliwa ubunge.

Hapa naona tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe,
Gharama za uchaguzi ziko juu sana, kurudia uchaguzi ni kujiingiza katika gharama ambazo tungeweza kuziepuka kama mamlaka husika zingeweza kusimamia vyema swala zima la Uchaguzi.

Mpaka sasa kuna wabunge wawili wamevuliwa Ubunge, Mmoja wa Chadema na mwingine wa CCM. Kwahiyo mpaka dakika hii ni ngoma Droo kwa vyama vyote.

Who do you think is in the loosing End up to this point?

Aah Vivian hapo kwenye Avata ni picha yako au? it look sweet lol!
 
Usisahau tu kuwa haki hupatikana kwa gharama vile vile. Unajua hao wanaotuingiza kwenye hizi gharama imewagharimu kiasi gani? Kinachotakiwa ni tume ifanye marekebisho ya sheria yao ya gharama za uchaguzi kuwa inapotokea mbunge anapoteza ubunge wake kwa kushindwa kesi mahakamani basi gharama zote za uchaguzi wa marudio ambazo zingelipwa na tume basi alipe huyo aliepoteza ubunge kama vile anavyotakiwa kulipia gharama zote za kesi alioshindwa. Kama mbunge atapoteza ubunge wake kwa kufukuzwa kwenye chama basi chama kilichomfukuza mbunge kiwe tayari kulipa gharama za uchaguzi utakaorudiwa vile vile mbunge au diwani anapokihama chama chake na hivyo kupoteza udiwani au ubunge wake sheria imtake kulipa gharama zote za uchaguzi wa marudio aliousababisha kwa sababu ya utashi wake wa kisiasa. Gharama za vyama na wagombea libaki kuwa kwa vyama na wagombea wao maana wana hiari ya kusimamisha mgombea au kutosimamisha.
 
Ni wazi kwamba Serikali hii ya Awamu ya Nne imekua na kesi nyingi za kupinga matokeo ya Ubunge kuliko serikali ya awamu yeyote ile katika Historia ya nchi yetu.

Kwa vile hapa jamvini kuna makada wa vyama tofauti, Tunashangalia pale Mbunge wa upande wetu ameshinda kesi au pale mbunge wa chama Pinzani amevuliwa ubunge.

Hapa naona tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe,
Gharama za uchaguzi ziko juu sana, kurudia uchaguzi ni kujiingiza katika gharama ambazo tungeweza kuziepuka kama mamlaka husika zingeweza kusimamia vyema swala zima la Uchaguzi.

Mpaka sasa kuna wabunge wawili wamevuliwa Ubunge, Mmoja wa Chadema na mwingine wa CCM. Kwahiyo mpaka dakika hii ni ngoma Droo kwa vyama vyote.

Who do you think is in the loosing End up to this point?

Mamito ungeweka statistics ungetusaidida zaidi or mwenye nazo plz..... by the way umepotea sana jukwaani hadi nikasema isijekuwa umeresti......lol...
 
Kuna matatizo mawili yaliyojitokeza kwenye hii awamu ya Nne

Moja ni Nguvu ya Dola inaweza kuchagua Mbunge au Rais kuliko Nguvu ya Kura za wananchi kwa kuiba masanduku au
Mipango Mingine ya kinyemelea

Tatizo lingine ni Uwezo wa Wabunge wetu kuwa na pesa za kuhonga wananchi wetu ambao wengi wana njaa, wanatumia uwezo huo wa kuwalisha, kuwapa vitu, ambavyo havita dumu maishani mwao lakini wamenunuliwa kumchagua mtu fulani hata kama hawampendi...

Wote hao wakiamka, wanaueleza Umma na Mbunge alieshindwa anakwenda Mahakamani - kwahiyo tatizo ni Ubwanyenye na Ukiritimba wa Mali ndio uliosababisha wengi kwenda mahakamani kudai haki zao za Ubunge kushindwa
 
Back
Top Bottom