Kesi ya Uhalali wa Muungano kuhamia The Hague

Kesi ya Uhalali wa Muungano kuhamia The Hague

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
Ile case ilioyofunguliwa na Wazanzibari 40,000 kudai uhalali wa Muungano (Jamuhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar) ambayo case hio ilikuwepo EAC Court tuna taarifa kusogea mbele kwa mbele.

Baada ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya waziri wa mambo ya nje kuiyandikia barua mahakama ya EAC kujitoa, imeipa uhalali na njia rahisi zaidi case hii ya madai ya wazanzibari kwenda kimataifa zaidi.

Sasa case hii kupelekwa international court of justice huko ulaya Netherlands [emoji1179].

Tunawaombea mafanikio mema Wazanzibari wenzangu, naamini haki itapatika Insha Allah
 
Balozi Seif Idd anawashangaeni sana kwani Muungano unawanufaisha zaidi ninyi wazanzibar!
Wazanzibar wakifanikiwa tutawachangia Wachagga wadai nchi yao ya Kilimanjaro

tz)chagg.jpg
 
Wazanzibari wanahaki ya kujitoa kwenye Muungano huu ulioasisiwa katika mito ya damu

Ni jambo la busara kupeleka kesi hiyo huko the Hague iwapo Wazanzibari watashinda basi mahakama itaauamuru Umoja wa Mataifa uitishe azimio la kura ya maoni

Swali linakuja je Wazanzibari wanataka Muungano ubaki lakini ubadilishwaje au uvunjwe kabisa?

Kama Wazanzibari wataamua kuachana na Muungano kabisa hilo swala litazigawa familia nyingi sana mfano mzuri ni Ethiopia na Eritrea

Mimi nimetembelea Visiwani mara kadhaa nimeshuhudia Wazanzibari wanaishi maisha ya mateso makubwa uonevu na Zulma ya kiwango ambacho unaweza kukifananisha na enzi za Jean Bedel Bokasa

Kama watachagua aina tofauti ya Muungano pia litakuwa jambo la busara kama Maalim alivyosema kuwa Muungano wa mkataba yote kheri

Hii zahma tumeletewa na CCM na tukiiondoa basi kila kitu kinawezekana bila hata ya kwenda Mahakamani

Kama tujuwavyo CCM ni kimbilio la wajinga na zama zake zimekwisha leo hii dunia ni kijiji kila kitu kiko wazi na wajinga wanazidi kuelimika

Nawatakia Wazanzibari kila la Kheri ili hatimae wawe na uwezo wa kujifanyia/kujiamulua maamuzi yao wao wenyewe
 
Hakuna ubishi wao ndio wanufaika zaidi wa
muungano sijuwi huwa ni wapi wana kwama
Wapemba biashara zao sijuwi zitakuwa katika hali gani muungano ukivunjika wakutane na jiwe tena wanafutiwa uraia siku moja wote!
Na uhujumu uchumi wa kiwango cha lami!
 
Hakuna ubishi wao ndio wanufaika zaidi wa
muungano sijuwi huwa ni wapi wana kwama
Wapemba biashara zao sijuwi zitakuwa katika hali gani muungano ukivunjika wakutane na jiwe tena wanafutiwa uraia siku moja wote!
Na uhujumu uchumi wa kiwango cha lami!
Hawa waliofungua kesi wasaidiwe kwa kadri tunavyoweza. Tumenyonywa kiasi cha kutosha.
 
Nje ya muungano hakuna Zanzibar bali kuna Unguja na Pemba kama nchi mbili tofauti. Najua issue kubwa inayowasumbua ni kutaka kuifanya zanzibar kuwa nchi ya ki-islam na kupata misaada toka kwa nchi za Ki-islam. Lakini hilo halitowezekana angalau kwa sasa.
 
Kuna taratibu za kupeleka kesi The Hague kwenye Mahakama ya Kimataifa ( International Court of Justice). Baadhi ya masharti kufungua kesi kwenye Mahakama hiyo ni yafuatayo:

a. Kesi inayofunguliwa huwe ni mgogoro baina ya mataifa yenye mamlaka kamili (Sovereign state) ni ukweli usiopingika nje ya Tanzania, Zanzibar si taifa lenye mamlaka kamili. Halitambuliki East Africa, SADC, AU na hata UN.

b. Hakuna mtu, watu au kikundi Cha watu chenye fursa ya kufungua kesi ICJ. Wanaodaiwa kuwa ni wanzanzibari wanapeleka kesi ICJ watapoteza pesa bure hawana haki ya kuwasilisha taifa kama wanna harakati.

c. Pande zinazohusika kwenye mgogoro lazima ziridhie mgogoro kupelekwa ICJ kwa usuluhishi. Hii Ina maana kwamba hata kama Zanzibar ingelikwenda kufungua kesi huko ICJ bado Tanzania hailazimishwi kuhudhuria kwenye usuluhishi pia maamuzi Mahakama hayatakuwa na nguvu juu ya Tanzania.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi zungumza na mtu fulani kuhusu muungano na nilimwambia kuwa tusipokuwa makini watanzania, wazungu watatugawa kupitia muungano kwani ndio suala pekee kubwa Lenye chanya ya mvurugano. China and Hong Kong walipounganishwa na waingereza dunia ilikaa kimyaaa.

China ilipopambana kujikwamua kiuchumi na kuwa Super Power nation in the economy of today, wameanza kumtumia Hongkong kama fimbo ya kuichapa China.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Zanzibar.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Balozi Seif Idd anawashangaeni sana kwani Muungano unawanufaisha zaidi ninyi wazanzibar!
Waliofilisika kisiasa huwa wanakimbilia kwenye udini ama ukabila.
Nakushauri jenga hoja isiyoegemea maeneo hayo kwa sababu wengi kati ya wazanzibar ni waislamu. Kuna ubaya gani kama wataomba msaada kutoka kwa waislamu wenzao?
Nje ya muungano hakuna Zanzibar bali kuna Unguja na Pemba kama nchi mbili tofauti. Najua issue kubwa inayowasumbua ni kutaka kuifanya zanzibar kuwa nchi ya ki-islam na kupata misaada toka kwa nchi za Ki-islam. Lakini hilo halitowezekana angalau kwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tunaweza kuamua juu ya hatma ya nchi yetu, kama tunataka tuwe na TZ ya namna gani.
Tulijaribu kuandika katiba mpya wakaja watu wakasema wao ndiyo pekee wenye uwezo na maamuzi juu ya nchi nzima.
Hawakutaka kusikiliza watz wasio na vyama wanataka nini
Leo wapo wachache wanaoamua hata kiongozi wa kijiji awe yupi
Mwishowe wengi wanaona nchi iko mikononi mwa wachache, wanaitawala nchi vibaya kuliko hata wakoloni wa kizungu.
Kinachofuata ni watu kutumia njia mbadala ili kuweka uongozi wanaoutaka.
Sisi yetu macho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom