Kesi ya Uchaguzi Igunga leo 25.07.2012

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746
kesi ya Uchaguzi Iliendelea jana (23.07.2012) katika mahakama ya Nzega, hatua iliyofikia ilikuwa ni Mh. J.P.Magufuri kujakutoa maelezo ya utetezi kuhusu tuhuma zinazomkabili za kutumia nafasi ya uwaziri katika kufanya kampeni kwa chama chake (CCM), cha kushangaza akuweza kutokeza mahakamani na maelezo yaliyotolewa ni kwamba ana ED ya mwezi mzima hivyo hawezi kufika hadi hapo ED itakapokwisha.

Uamuzi wa JAJI amewapa CCM masaa 48 tangu jana Magufuri awe amefika kutoa maelezo yake ya utetezi wasipofanya hivyo ndiyo itakuwa mwisho na tarehe ya Hukumu itapangwa.

My Take
Hii si inaonyesha Dharau kwa mahakama? kama ana ED mbona Bungeni anahudhuria, kwa mnao jua sheria kwa mtu kama huyu anayedharau mahakama huwa anachukuliwa hatua gani?

Mwendelezo:-
Baada ya Mh. Mgufuli kupewa masaa 48 awe amekuja kutoa maelezo amekaidi amri hiyo na inasemekeana amesema hawezi kuja kutoa maelelzo kama uchaguzi kurudiwa na urudiwe. Jaji ameamua kusitisha utetezi huo na kuhairisha kesi hadi tarehe 20.08.2012 ambayo ndiyo itakuwa siku ya hukumu.

Kabla ya kutoa uamuzi huo alipokea barua kutoka kwa wanasheria wa mlalamikaji kuhusiana na kietendo cha ukaidi wa Mh. Magufuli.

NB:Katika kesi hii Kafumu amekuwa akilalamika kutengwa na CCM katika suala zima la kesi kiasi imebidi atumie fedha zake katika gharama za uendeshaji wa kesi kwa watu wa upande wa CCM na isitoshe kitendo cha Magufuli kutokuja kutoa maelezo kimemuhudhunisha sana na kumkatisha tamaa na hususani kauli ya kusema kama kurudiwa uchaguzi na urudiwe, kiasi amesikika akisema anajilaumu kwa kuacha Ukamishna na kukimbilia Ubunge.

KESI KWA UPANDE WA CCM IMEWAKALIA VIBAYA LABDA ICHAKACHULIWE.
 
Imekula kwao magamba mungu akiwa upande wetu hakuna alie juu yetu
 
Imekula kwao magamba mungu akiwa upande wetu hakuna alie juu yetu
penye haki always uongo hujitenga. tulianza na MUNGU na mpaka 2015 tutamaliza na MUNGU.
 
Kwa niliyoyaona segerea hapa hamna kesi ya kushiinda ccm
 
Mwingulu Nchemba uchaguzi huo unakuja igunga sijui umejiandaa kuuwa makada wa chadema wangapi safari hii maana unahasira kweli safari hii.....
 
Anajuta kuacha ukamishna wa madini, na nafasi wameshachukua wengine, posho za bungeni anazitumia kuwalipa mashahidi. Liwe funzo kwa wanaCCM wenzake ambao hawajatambua kuwa chama lao halina nafasi tena. Thanks Kibogo for updates. Walau umetutoa kwa wataka urais.
 
Kwa niliyoyaona segerea hapa hamna kesi ya kushiinda ccm

Sitaki kuamini kuwa majaji wote ni voda fast, sijui uadirifu wa jaji anae simamia kesi ya igunga....labda mwenye CV yake atuwekee vinginevyo tusitalajie jipya.....
 
Tunataka tuone haki ikitendeka katika maamuzi. Magamba kwishney!
 
Mwingulu Nchemba uchaguzi huo unakuja igunga sijui umejiandaa kuuwa makada wa chadema wangapi safari hii maana unahasira kweli safari hii.....
As we move forward, anaweza kujikuta yeye ndiye anachinjwa. Sasa hivi watu wana hasira sana na CCM, na ili kulijua hili wajichanganye na watu wa kawaida au waitishe mikutano ya hadhara waone muitikio.
 
Yan magamba wameshikwa pabaya!
 
Mungu asimamie ili hakimu amue kwa haki na sikwamatakwa ya watawala
 
Msifurahie sana ya magufuli hizi mahakama za kisisiem hazina adabu ,cha msingi tulie na tume huru ya uchaguzi,hata ziitishwe chaguzi kumi leo haki ya kushinda ni finyu sana.sisiem wako radhi wafungue hazina watoe pesa yote ili washinde
 
Mwingulu Nchemba uchaguzi huo unakuja igunga sijui umejiandaa kuuwa makada wa chadema wangapi safari hii maana unahasira kweli safari hii.....



Mkubwa! Wao wana pesa Sisi tuna MUNGU aliye hai sasa na hata milele!

Tutajua jeuri yao iko wapi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…