Kesi ya Naibu Rais wa Kenya yaendelea

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
Kesi ya uhalifu inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ya The Hague hatimaye imeanza.

Ruto yuko katika mahakama hiyo na mwandishi Joshua Arap Sang ambaye pia anajaribu kutoa ushahidi utakaosababisha kufutiliwa mbali kwa kesi hiyo inayohusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Mnamo mwezi Disemba mwaka jana mahakama hiyo ilifutilia mbali mashtaka dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa ukosefu wa ushahidi,lakini mwendesha mashtaka anahoji kwamba bwana Ruto na mwandishi Joshua Sang wana kesi ya kujibu.

Washtakiwa wanasema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea huku wakikana mashtaka hayo.

Chanzo: BBC
 
Last edited by a moderator:
Kenyatta alichomokaje? Au ukiwa rais tazama yamekuwa mapya wala makosa yako hayatokumbukwa tena?
 
Kenyatta alichomokaje? Au ukiwa rais tazama yamekuwa mapya wala makosa yako hayatokumbukwa tena?
Aliyekwambia Kenyatta alikuwa na makosa ni nani?Wapi kina Mwai Kibaki na Raila Odinga?Mbona hawakufikishwa ICC wakati hao ndio walioleta vurugu hiyo yote?Huelewi siasa wewe!
 
Aliyekwambia Kenyatta alikuwa na makosa ni nani?Wapi kina Mwai Kibaki na Raila Odinga?Mbona hawakufikishwa ICC wakati hao ndio walioleta vurugu hiyo yote?Huelewi siasa wewe!
We Mende huelewi ICC kesi zinapelekwa na wananchi wenyewe? Why not ask your 'fellow' kenyans why Ruto and not Mwai?
 
We Mende huelewi ICC kesi zinapelekwa na wananchi wenyewe? Why not ask your 'fellow' kenyans why Ruto and not Mwai?
We burukenge umejua Ocampo alitoa majina ya watu sita aliyeamua wana kesi ya kujibu?Mambo ya Waki report unaelewa wewe,au hata kushirikishwa kwa NGO's za Kenya kutafuta mashahidi?Soma kwanza kijana.
 
We burukenge umejua Ocampo alitoa majina ya watu sita aliyeamua wana kesi ya kujibu?Mambo ya Waki report unaelewa wewe,au hata kushirikishwa kwa NGO's za Kenya kutafuta mashahidi?Soma kwanza kijana.
Wewe mende ndio unatakiwa usome jinsi kesi zinavyopelekwa ICC. Wacha kudandia mambo kwa mbele. Kama hata hujui FACT kwamba Tanzania ndio iliyosuluhisha kenya why bother with vitu vikubwa kwako kama ICC? Mende mkubwa wewe once again!
 
Back
Top Bottom