Kesi ya Mdee, Kubenea yapigwa kalenda

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
KESI ya shambulio inayowakabili Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo na Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga imeahirishwa leo katika Mahakama ya Kisutu kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha upelelezi,

Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Shafii Juma, mfuasi wa Chadema; Manase Mjema, Diwani wa Kimanga pamoja na Alfonce Kinyafu, Diwani wa Kimara Saranga ambao kwa pamoja wanadaiwa kumshambulia Theresia Mmbando, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa harakati za Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Helleni Liwa, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ameahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 2 Juni mwaka huu.

Mdee, Waitara, Shafii na Kinyafu walifikishwa mahakamani hapo tarehe 2 Machi mwaka huu ambapo Kubenea na Mjema wakifikiswa 11 Machi.
 
imebaki hiyo tu na kujirekodi maana bila hayo wengine tutawapiteza kabisaa
 
Back
Top Bottom