Kesi ya Mbunge wa CUF Yatikisa Tanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Mbunge wa CUF Yatikisa Tanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Nov 11, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  na Mwandishi Wetu, Tanga

  KUNDI kubwa la wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Tanga likiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, jana asubuhi walifurika katika viwanja vya mahakama ya wilaya hiyo kusikiliza mwenendo wa kesi inayomkabili Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho mkoani hapa, Nuru Bafadhili na viongozi wengine watano.
  Watuhumiwa wengine ni Rashid Jumbe, Diwani wa Kata ya Mwanzange (CUF), Mussa Mbarouk Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini (CUF), Abdulrahman Hassan, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Amina Yusuph na Mohamed Asilia, ambao walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali pamoja na kutoa maneno ya kumkashifu Rais Jakaya Kikwete.
  Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 27 mwaka huu, majira ya saa 10 hadi saa 12 jioni katika eneo la Chuda, mjini hapa.
  Mbele ya Hakimu mkazi, Laurent Mbuya washitakiwa hao walisomewa mashitaka matatu tofauti ya kula njama kwa kutenda kosa, kukusanyika bila kibali na kutumia lugha ya kashfa kinyume cha sheria. Hata hivyo walizikana tuhuma hizo.
  Wakati kesi hiyo ikitajwa jana, Mwendesha Mashitaka, Wakili wa Serikali, Omari Kibwana aliiomba mahakama hiyo kufuta dhamana ya mtuhumiwa wa kwanza, Nuru Bafadhili, kwa madai kuwa ameshindwa kufika mahakamani hapo wakati kesi hiyo ilipotajwa mara ya mwisho.
  Hata hivyo, Hakimu Mbuya alimtaka mtuhumiwa aieleze mahakama sababu zilizomfanya kutohudhuria mahakamani ambapo alidai alikuwa mjini Dodoma kuhudhuria mkutano wa 17 wa Bunge. "Mheshimiwa Hakimu ni kweli tarehe iliyopita sikufika mahakamani lakini niliandika barua ya kujieleza na nilimwomba mdhamini wangu afike mahakamani kuniwakilisha kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge," alidai mbunge huyo. Kesi hiyo imeahirishwa tena hadi Desemba 8, mwaka huu na kwamba ushahidi bado haujakamilika wakati watuhumiwa wataendelea kuwa nje kwa dhamana

  source:TANZANIA DAIMA
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  CCM bana aaaaaaaaaaaagh!!!
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapo sasa ndio panachanganya. Wapinzani wakifanya mkusanyiko wowote wa kujadili mambo yao mara kwa mara polisi huita kitendo hicho "HARAMU" Kitendo hichohicho kikifanywa na CCM ni halali kabisa ila wamekosea kidogo, wataambiwa baadaye wafuate utaratibu. Wapinzani hawana kuambiwa wmekosea kidogo. Kuwa mpinzani nchi hii ni kama uhaini vile. Ndio maana ni vigumu nchi hii ikacheza fair play in politics.

  Leka
   
Loading...