Kesi ya mbunge Bilago(CDM ) yapigwa tarehe

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,188
570
Kesi ya Chiza na mbunge Bilago imeahirishwa mpaka tarehe 5/4/2016 hii inafatia upande wa walalamikaji kuomba mda wa kuanda ushahidi na mashahidi wao

Hoja anazolalamikia Chiza ambaye pia alikuwa waziri wa Kilimo na mbunge wa CCM jimbo la Buyungu 2010_2015 na kushindwa vibaya uchaguzi uliyoisha ni hizi

1:Anamshataki msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo la Buyungu na mwanasheria wa serikali.
2:Anapinga matokeo ya vituo 13 kati ya 16

3:Kwamba kuna mpiga kura wake alipigwa na kutishiwa maisha wakati wa kampeni na timu kampeni ya Bilago.

4:Kwamba kuna afsa ugani wa serikali akimsaidia Bilago kampeni.

5:Kwamba kuna mwalimu alimpigia kampeni Bilago na kumsababishia yeye kupoteza kura kinyume na sheria za utumishi.
mahakama imeagiza tarehe hiyo mambo yote yawe yamekamilika na kwamba itaaanza kusikilizwa mfululizo mpaka mwisho.
 
Back
Top Bottom