Kesi ya Mbowe, wenzake yaanza kusikilizwa

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
kesi-ya-mbowepic.jpg

Dar es Salaam. Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi leo imeanza kusikilizwa mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.

Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani hapa saa 3:00 asubuhi leo Ijumaa Septemba 3, 2021 wakisindikizwa na askari wa jeshi la Magereza wenye silaha.

Baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama, Mbowe na wenzake wamshushwa kwenye basi la Magereza na kwenda na kuingizwa mahakamani.

Tayari Jaji Elinazer Luvanda anayesikiliza kesi hiyo ameshaingia mahakamani.

Leo kesi hiyo inaendelea katika hatua ya usikilizwaji wa pingamizi la awali lililowekwa na washtakiwa kupitia kwa jopo la mawakili wao 14 wakiongozwa na Peter Kibatala.

Katika pingamizi hilo washtakiwa hao wanadai kuwa hati ya mashtaka ina kasoro za kisheria pamoja na mambo mengine wakidai kuwa sheria ya ugaidi ambayo wanashtakiwa nayo haijafafanua viambato vya kosa la ugaidi na kwamba upande wa mashtaka haujazingatia masharti ya lazima ya sheria hiyo ambayo ni kueleza kusudio la vitendo vya ugaidi ambavyo washtakiwa wanatuhumiwa kuvitenda.

Tayari mawakili wa Serikali wakiongozwa na wakili wa Serikali mwandamizi, Robert Kidando wameanza kujibu hoja za utetezi za pingamizi hilo zilizotolewa na mawakili wa utetezi juzi Jumatano Agosti 31,2021.

Serikali inawakilishwa na timu ya mawakili watano.

Washtakiwa ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa, Mohamed Abdallah Ling'wenya na Mbowe.

Chanzo: Mwananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom