Kesi ya Lema: Upande wa Serikali wapinga Rufaa, arudishwa rumande

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,279
Rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ya kupinga kunyimwa dhamana inatarajiwa kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Wananchi wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi mahakamani ili kumtia moyo Mbunge wenu Godbless Jonathan Lema.

PICHA: Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akishuka kwenye gari la mahabusu alipowasili kwenye viwanja vya mahakama kusikilizwa kwa rufaa yake ya kupinga kunyimwa dhamana mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Leo..
FB_IMG_1482908721598.jpg
FB_IMG_1482908728094.jpg


==============

Usikilizwaji wa Rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ya kupinga kunyimwa dhamana imekwama kusikilizwa baada ya upande wa Jamhuri kukata rufaa ya kupinga mbunge huyo kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi ya rufaa.

Lema aliyekamatwa Novemba 2, akiwa mjini Dodoma tangu wakati huo anashikiliwa kwenye gereza la Kisongo jijini Arusha.

Baada ya rufaa ya Lema kukwama leo amerudishwa gereza la Kisongo.

Leo zimetajwa kesi mbili, ambazo ni ile ya Criminal Apeal namba126, Godibless Lema vs Jamhuri na ile ya

Criminal Apeal namba135, Jamhuri vs Godbless Lema.

Ambapo Upande wa utetezi umekuja na maombi kuwa isikilizwe Ile rufaa ya serikali kwanza, Criminal Apeal namba135. Kwahiyo maelekezo wameambiwa serikali iwasilishe notice of appeal kesho alhamisi, kisha ijibiwe kesho kutwa Ijumaa. Then, ijibiwe na Jamhuri tarehe 02/01/2017. Na Tarehe 04/01/2017 itolewe uamuzi..!!!!

Wakuu,

Leo Mawakili wa Serikali kwenye kesi ya Lema wamewasilisha Rufaa ya kuipinga Rufaa hiyo hivyo kisheria inabidi wasikilizwe wao kwanza.

Kwa maana hiyo, ruling ya rufaa ya Lema itatolewa tarehe 04 Januari 2017.

Lema karudishwa rumande.



Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza rufaa mbili,Jamuhuri dhidi ya Mhe.Godbless Lema(CRIMANAL APPEAL NO 135) na Rufaa ya Upande wa Utetezi(CRIMINAL APPEAL NO 126),Rufaa zote mbili zinapinga maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi yaliyotolewa tarehe 11-11-2016.

Aidha shauri la Rufaa ya Jinai Jamuhuri dhidi ya Lema (CRIMINAL APPEAL NO 135) linapinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi kumpa Lema dhamana na Shauri la Rufaa ya upande wa utetezi (CRIMINAL APPEAL NO 126) linapinga kitendo cha Mahakama ya Hakimu Mkazi kumpa lema dhamana pasipo kuweka masharti ya dhamana.

Hata hivyo Jopo la Mawakili wasomi wa upande wa utetezi wakiongozwa na Peter Kibatala aliiomba Mahakama kuu isubirishe kwanza Rufaa yao na ianze kusikiliza Rufaa iliyowasilishwa na Jamuhuri jambo ambalo halikupingwa na wakili wa upande wa jamuhuri.

Pia wakili mwandamizi wa serikali ndugu Inocent Njau aliiomba Mahakama hiyo kuwasilisha hoja za rufaa yao kwa njia ya maandishi jambo ambalo liliridhiwa na Jopo la mawakili wasomi wa upande wa utetezi (DEFENSIVE COUNSEL)

Baada ya Majibizano hayo Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Mhe.Salma Mussa Maghimbi ameamuru upande wa Jamuhuri kupeleka hoja zao kwa maandishi tarehe 29-12-2016 na upande wa utetezi(Defensive Counsel) nao watajibu hoja zao kwa maandishi(Writing Submission) tarehe 30-12-2016,Upande wa Jamuhuri watajibu tena hoja zao kwa maandishi(Rejoinder) tarehe 02-01-2017

Mhe.Jaji atatoa uamuzi siku ya Jumatano tarehe 04-01-2017.
 
Rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ya kupinga kunyimwa dhamana inatarajiwa kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Wananchi wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi mahakamani ili kumtia moyo Mbunge wenu Godbless Jonathan Lema.
Tunakuja kwa wingi kumpokea wakati anatoka kwa dhamana
 
Atatoka siku watesi wake wakijisikia. Sijui wanasubiri mpaka wakapigiwe magoti?

Yaani dhamana tu? As if mtu yupo anaomba kufutiwa kesi! Harafu hao hao kila Jumapili/Ijumaa wanawahi viti vya mbele/mikeka ya mbele ili mapadre/mashekhe wawaone na kuwabariki. Mungu/Allah Subhana wa Taalah sio fala kihivyo.
 
Back
Top Bottom