Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,035
- 144,400
Kesi kuanza kusikilizwa kesho
kesi ya kupinga wagombea wanaopita bila kupingwa kutangazwa washindi bila kupigiwa kura kuanza kusikilizwa kesho
a uliopo sasa unaoruhusu mgombea aliyeteuliwa na mamlaka za uchaguzi, kuwa mgombea pekee na kutangazwa kuwa 'amepita bila kupingwa' kutokana na sababu mbalimbali za kisheria, imepangwa kuanza kusikilizwa siku ya Jumanne, Septemba 3, 2019 mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Shauri hilo ambalo limesajiliwa rasmi wiki iliyopita Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dar es Salaam kwa kupewa namba 20/2019, litakuwa mbele ya majaji; Feleshi J, Masoud J na Maige J, ambapo mpeleka maombi Wakili Gaston Shundo Garubindi anaiomba Mahakama kuu itamke kuwa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na kifungu cha 45(2) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (uchaguzi) Sura ya 292, vinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa maombi hayo, vifungu hivyo (44 na 45(2) vya sheria hizo mbili ambazo zinasimamia Uchaguzi Mkuu (Rais na wabunge) na Uchaguzi wa Madiwani mtawalia, na kuruhusu mamlaka ya uchaguzi kumtangaza mgombea pekee kuwa mshindi wa nafasi aliyogombea, bila kupigiwa kura na wananchi wa jimbo au kata husika kwa sababu ni mgombea pekee katika nafasi husika (kupita bila kupingwa), vinakiuka ibara ya 21 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Itakumbukwa kuwa Ibara ya 8 ya Katiba ya Nchi inazungumza kuwa Serikali itapata mamlaka yake kutoka kwa watu, huku ibara ya 21 ikielekeza kuwa watu wote wana haki ya kushiriki katika masuala ya utawala wa nchi, ikiwa ni pamoja na shughuli za uchaguzi ambao unahusisha haki ya kupiga kura na kupigiwa kura. Hivyo kutekelezwa kwa vifungu vya sheria hizo, si tu kunawanyima wananchi haki ya kikatiba ya kupiga kura na kupigiwa kura, bali pia kunaweka mazingira ya wananchi kutawaliwa na mamlaka ambazo hazijatokana na wao, kama Katiba inavyoagiza.
Wajibu maombi katika shauri hilo, ambao tayari wameshapelekewa na kupokea wito wa Mahakama Kuu ni; Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Maombi ya shauri hilo na. 20/2019 yamewasilishwa mahakamani hapo chini ya hati ya dharura na yamepangwa kuanza kusikilizwa kesho saa 3 asubuhi.
Imetolewa leo Jumatatu, Septemba 2, 2019 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema