PostGE2025 Kesi ya Kupinga Tume Ya Jaji Chande kusikilizwa Desemba 12

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam Ijumaa hii ya Desemba 12.2025 majira ya saa 08 mchana inatarajiwa kusikiliza kesi Na. 30210/2025 iliyofunguliwa na Mwanaharakati Rosemary Mwakitwange na wenzake wawili (2) ambao ni Mawakili Deogratias Mahinyila na Edward Heche dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Wajumbe Nane wa Tume Huru ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini Oktoba 29 na siku zilizofuata, sambamba na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)

Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Jaji Hussein Salum Mtembwa leo, Jumatano Desemba 10.2025 imekuja kwaajili ya kutajwa ambapo waleta maombi wamewakilishwa na Mawakili Mpale Mpoki na Hekima Mwasipu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Tume hiyo wamewakilishwa na Mawakili wa Serikali Wakuu Narindwa Sekimanga na Erigh Rumisha, huku TLS ikiwakilishwa na Wakili Ferdinand Makore

Katika kesi hiyo, waleta maombi wanapinga uteuzi wa Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, ambapo miongoni mwa sababu zilizowasukuma kupinga uteuzi wa Tume hiyo ni kutokana na madai ya kutokuwa huru, kuundwa kinyume na sheria, madai ya kuundwa kwa nia mbaya, Tume kukosa mantiki ya kisheria kwa uundwaji wake nk,

Wakiwa Mahakamani hapo, Mawakili Hekima Mwasipu na Ferdinand Makore wakawaeleza Wanahabari kile kilichojitokeza leo.

Pia Soma: Kesi ya kupinga tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29 inaendelea leo Desemba 10
 
Wakili Hekima Mwasipu

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam inatarajia kusikiliza kesi Na. 30210/2025 ya kupinga uundwaji wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliytokea Oktoba 29, 2025, ifikapo Desemba 12, 2025.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Mwanaharakati Rosemary Mwakitwange na wenzake wawili (2) ambao ni Mawakili Deogratias Mahinyila na Edward Heche, imefunguliwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wajumbe wa Tume hiyo na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).

Leo Desemba 10, kesi hiyo ilikuja kutajwa mbele ya Jaji Hussein Salum Mtembwa, ambapo waleta maombi wamewakilishwa na Mawakili Mpale Mpoki na Hekima Mwasipu na kwa upande wa walalamikiwa yaani Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Tume hiyo wamewakilishwa na Mawakili wa Serikali Wakuu Narindwa Sekimanga na Erigh Rumisha, huku TLS ikiwakilishwa na Wakili Ferdinand Makore.

Katika kesi hiyo, waleta maombi wanapinga uteuzi wa Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, ambapo miongoni mwa sababu zilizowasukuma kupinga uteuzi wa Tume hiyo ni kutokana na madai ya kutokuwa huru, kuundwa kinyume na sheria, madai ya kuundwa kwa nia mbaya, Tume kukosa mantiki ya kisheria kwa uundwaji wake.

Tume hiyo iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan Novemba 18, 2025.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam Ijumaa hii ya Desemba 12.2025 majira ya saa 08 mchana inatarajiwa kusikiliza kesi Na. 30210/2025 iliyofunguliwa na Mwanaharakati Rosemary Mwakitwange na wenzake wawili (2) ambao ni Mawakili Deogratias Mahinyila na Edward Heche dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Wajumbe Nane wa Tume Huru ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini Oktoba 29 na siku zilizofuata, sambamba na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)

Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Jaji Hussein Salum Mtembwa leo, Jumatano Desemba 10.2025 imekuja kwaajili ya kutajwa ambapo waleta maombi wamewakilishwa na Mawakili Mpale Mpoki na Hekima Mwasipu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Tume hiyo wamewakilishwa na Mawakili wa Serikali Wakuu Narindwa Sekimanga na Erigh Rumisha, huku TLS ikiwakilishwa na Wakili Ferdinand Makore

Katika kesi hiyo, waleta maombi wanapinga uteuzi wa Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, ambapo miongoni mwa sababu zilizowasukuma kupinga uteuzi wa Tume hiyo ni kutokana na madai ya kutokuwa huru, kuundwa kinyume na sheria, madai ya kuundwa kwa nia mbaya, Tume kukosa mantiki ya kisheria kwa uundwaji wake nk,

Wakiwa Mahakamani hapo, Mawakili Hekima Mwasipu na Ferdinand Makore wakawaeleza Wanahabari kile kilichojitokeza leo.

Pia Soma: Kesi ya kupinga tume ya kuchunguza matukio ya Oktoba 29 inaendelea leo Desemba 10
Wekeni ushahidi lkn hamna kitu hapo. Hakuna Jaji wala mahakama hapo
 
Ile ya kupinga kutofanya Sherehe za Uhuru imeishia wapi? Mnatupeleka peleka tu...!
 
Back
Top Bottom