RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
April 01 2016 Serikali iliwapandisha kizimbani kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ Harry Kitilya, mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996 ambaye pia alikuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania Shose Sinare na Sioi Solomoni kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kula njama kutenda kosa pamoja na kosa la kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Kesi hiyo ilipangwa kuendelea tena leo April 22 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo imeahirishwa na Hakimu Mkazi Emillius Mchauru kwa sababu hakimu hajakamilisha uandikaji wa uamuzi wa kuondoa shitaka la utakatishaji fedha linalowakabili washtakiwa wote watatu. Kesi hiyo itaendelea tena April 27 2016 na watuhumiwa wamerudishwa rumande.