Kesi hizi zilikuwa na malengo maalum.
1. Kurudisha imani kwa wahisani ili misaada isikatwe.
2. Kuwatuliza wananchi wenye hasira dhidi ya watawala kwa kisingizio " Sheria iachwe ichukue mkondo wake"
Hata washitakiwa wenyewe wameishahakikishiwa kuwa hafungwi mtu wasiwe na wasiwasi Ili mradi serikali ya CCM ipo madarakani basi watalindwa.
Kuhusu tufanye nini hakuna la kufanya jamaa wameshika kotekote kwenye makali wameshika nchani kwa glove na kuachia katikati na kwenye mpini wameushika imara ili tukidanganyika na kushika makali yaliyoachwa wazi wanaanchia ncha na kuvuta kwa nguvu. Cha kufanya ni kuchukua jiwe na kupiga kwa nguvu kwenye glove ili ncha ipenye. Na hii itafanyika kwa njia moja tu, nayo ni kuwakosesha usingizi. Katiba ibadilishwe, Tume huru ya uchaguzi ila haya hayaji kwa kuongea huku ukiwa ndani unakula udaga na kauzu. Mfano mzuri Kenya.