GE2025 Kesi ya CHADEMA kuhusu mgawanyiko wa mali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Bodi la Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inaendelea leo, Jumatano Septemba 10.2025 kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam chini ya Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo

Soma pia: BUSARA: Freeman Mbowe jitokeze kuonesha mshikamano wa CHADEMA katika Kesi inayomkabli Lissu. Kushiriki kwako kutaponya mgawanyiko uliojitokeza

Your browser is not able to display this video.


Kutoka kwenye chumba namba mbili cha Mahakama hiyo tunakusogezea habari picha kuona namna Mawakili, viongozi na makada wa chama hicho walivyojitokeza, na kwamba wapo tayari kwa ajili ya kuanza kusikiliza mwendelezo wa kesi hiyo

Kesi hiyo inakuja leo kwa ajili ya usikilizwaji, ambapo tamati yake Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi endapo upande wa wadaiwa (Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA) wakabidhi nyaraka muhimu zilizoombwa na wadai (Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili) Mahakamani hapo

Itakumbukwa kuwa upande wa wadai waliomba Mahakamani hapo kupatiwa nyaraka kadhaa muhimu za kiutendaji za CHADEMA ikiwemo muhtasari na ajenda za vikao vya Bodi ya Wadhamini, Kamati Kuu, Sekretarieti ya chama, Sekretarieti maalum ya Zanzibar, Kamati maalum ya Kamati Kuu Zanzibar, taarifa za fedha nk

Maombi hayo yalipingwa vikali na upande wa wadaiwa, na leo Mahakama itasikiliza na kutoa uamuzi endapo wakabidhiwe nyaraka hizo au la

Ikimbukwe kuwa katika kesi ya msingi wadai wamelalamikia kuwa chama hicho kikiendesha shughuli zake pasipo kuzingatia usawa baina ya Tanzania Bara na Zanzibar, hiyo ikienda sambamba na mgawanyo wa mali, fedha, watumishi nk jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya CHADEMA, Katiba ya Tanzania na Sheria ya Vyama vya Siasa

Madai yao mengine ni pamoja na kutozingatiwa kwa usawa wa kijinsia, uwepo wa viashiria vya udini nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…