Kesi ya bihondo isichakachuliwe

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
KESI YA BIHONDO ISICHAKACHULIWE

Natumia fursa hii kwa mara nyingine kutoa Pole kwa familia ya marehemu Bahati Stephano aliyekuwa katibu wa Kata ya Isamilo na Kada wa CCM huko Mwanza.

Katika hali ya kushangaza siasa za Ukanda huo wa ziwa ni kama za visasi zaidi kuliko kutekeleza sera za vyama vyao na kuwatumikia wananchi. Sasa tunasikia sakata la Kamani na Chegeni ambalo nalo chanzo na hatima yake wanajua CCM wenyewe.

Nirejee kwa Ndugu Bihondo ambaye alianza siasa miaka ya 90 kama mtu aliyekuwa anajaribu hivi kusaka udiwani kata ya Isamilo, kama ngekewa akashinda.

Kuingia Halmashauri, madiwani wote form 4 na darasa la saba kasoro yeye aliyekuwa ameosha nyota kidogo katika uwanja wa elimu akaukwaa Umeya, tokea hapo roho ya ubinafsi, uchu wa madaraka na tamaa ya kujilimbikizia mali ikatawala hisia zake baada ya kuonja asali ya uongozi. Kama tujuavyo kwa Tanzania ukikamata madaraka ni zaidi ya mfanyabishara mahiri.

Huyu jamaa alipanda haraka na kukwaa nafasi nyingi ikiwemo ya Mwenyekiti wa ALAT taifa, sasa yupo huko gereza la Butimba wilaya ya Nyamagana akisubiri hatima yake.

Lakini mwendo wa kusuasua wa kesi hii tofauti na zilivyo nyingine toka May 2010 inaashiria njama za wazi kabisa kupindisha maamuzi na hatimaye huyu jamaa kuwa huru.

Inashangaza kuona upelelezi unachukua miaka sasa, na cha ajabusiku hiyo hiyo ya Tukio tu mtuhumiwa namba moja na mtekelezaji wa mauji hayo alimtaja on spot kuwa alitumwa na nani na kwa ujira upi na alishirikiana na akina nani ambao wote walipatikana kiurahisi kama unamkamata panya katika tundu.

Hofu yetu ni hii kasi ya utekelezaji wa upelelezi na kwa jinsi siasa hizi za chuki zinavyozidi kushamiri katika eneo la Ukanda wa Ziwa eneo lenye wapiga kura wengi Tanzania pengine kuliko pengine ukanda wowote ule.

Kauli mbiu yangu katika waraka huu, Haki itumike katika kesi hii kama itakavyofanyika kwa Kamani na wengine wote wanaokabiliwa na tuhuma za kesi za mauji, kama kweli alihusika na njama za kutaka kumuua Masunga Raphael Chegeni naye aadhibiwe kwa stahili yake licha kusuasua kwa polisi kumkamata kama walivyofanya kwa haraka kwa Kiongozi wa upinzani licha ya kuwa na Kinga ya Bunge.

Maamuzi ya Haki yatasaidia kukomesha mchezo huu mchafu wa wanasiasa walafi ambao wao Tanzania ni yao na serikali shemeji yao.



Nawasilisha
Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom