Kesi maarufu ya Ryland v Fletcher (1868)

Apr 26, 2022
64
100
Hii ni kesi maarufu sana kwenye sheria ya madhara (Law of Tort) , ambayo imeanzisha kanuni (Rule au Principle) moja muhimu sana, inayojulikana kama STRICT LIABILITY.

STRICT LIABILITY, ina maana mtu anawajibika kwa adha au madhara aliyoyasababisha bila kujali alidhamiria au la (MENS REA/INTENTION), na bila kujali kama kuna uzembe wowote amefanya au la (NEGLIGENCE)!

Ikishabainika tu kwamba umefanya kosa (ACTUS REUS), basi hayo mengine yote ni IRRELEVANT. No need to establish Intention or negligence on the part of the defendant. Hii ndio inaitwa "STRICT LIABILITY (NO FAULT LIABILITY)."

Sasa hii kesi inahusu ADHA (NUISANCE):

NUISANCE (ADHA) ni mtu au kitu kinachosababisha (kuleta) kero, usumbufu au shida.

Au (nuisance) ni kitendo cha mtu kufanya kitu kisichoruhusiwa na sheria au kuacha kufanya wajibu wake kisheria, na hatimaye anasababisha madhara au kero au usumbufu au taabu kwa watu wengine katika kufurahia haki zao. Anafanya maisha yawe magumu.

Mfano harufu mbaya, moshi, mwanga mkali, kufungulia mziki sauti kubwa (makelele), n.k

Sasa, Kesi ya RYLANDS V FLETCHER ilileta mabadiliko makubwa sana kwenye sheria ya madhara hasa kipengele cha ADHA (NUISANCE). Ilitoa mwongozo wa namna ya kumwajibisha mtu anayeleta au kusababisha kero kwa wengine.

MATERIAL FACTS (STORI YA KESI):

Mlalamikaji (Plaintiff) kwenye hii kesi alikuwa Thomas Fletcher, mmiliki wa mgodi na Mshtakiwa (Defendant), alikuwa Rylands, aliyejenga bwawa la maji kwenye kiwanja chake.

Sasa Thomas Fletcher (Mlalamikaji) alikuwa amekodi migodi ya makaa ya mawe, kwenye eneo lililokuwa limepakana na kiwanja cha Rylands (Mshitakiwa).

Rylands alikuwa anamiliki mashine. Rylands akatafuta mafundi (wakandarasi) akawalipa pesa, wamjengee kwenye kiwanja chake, hifadhi ya maji (kingo za kutunzia maji, au naweza kuita bwawa) ili iwe inatumika kusaidia kusambaza maji kwenda kwenye mashine yake hiyo.

Rylands mwenyewe hakuwa amehusika kwenye huo ujenzi, ila aliingia tu mkataba na hao mafundi (wakandarasi/wahandisi) mahiri/bora kabisa wenye vigezo, na kuwalipa wajenge.

Wakiwa katika ujenzi, wakandarasi waligundua ardhini mashimo kadhaa ya zamani ya makaa ya mawe yaliyokuwa yamezibwa juu juu tu, kwa mchanga na kifusi (udongo), ambayo (mashimo hayo) yalikuwa yamepakana au yako Karibu na mgodi wa mlalamikaji (Thomas Fletcher) ambao ulikuwa karibu/kando na eneo hilo.

Sasa, badala wayazibe hayo mashimo, wakandarasi wakayaacha kama yalivyo.

Kiufupi, wakandarasi wakiwa wanachimba ili wajenge bwawa la maji, walikutana na mashimo ya migodi ya zamani ambayo haitumiki, ila wakashindwa kuyaziba ipasavyo (UZEMBE/NEGLIGENCE).

Kwa hiyo, hifadhi hiyo ya kutunzia maji au bwawa, ikawa imejengwa juu ya mashimo ya migodi hiyo ya zamani ambayo ilikuwa haitumiki.

Ryland hakuwa na habari/hakujua kuwa bwawa limejengwa juu ya mashimo hayo! Ila mafundi (wakandarasi) walijua lakini wakamficha, wasimwambie lolote! Na Ujenzi ulipokamilika WAKAJAZA MAJI LILE BWAWA.

Ilikuwa Tarehe 11 December 1860, muda mfupi tu baada ya kuwekwa maji kwa mara ya Kwanza, hifadhi hiyo ya maji ya Rylands (bwawa) ILIPASUKA na kuugharikisha (kufurika) maji mgodi wa Fletcher.

Yaani Kutokana na ule uzembe wa mafundi/wakandarasi, maji yakahama kutoka kwenye lile bwawa na kujaa kwenye mgodi wa Fletcher uliokuwa jirani na kupelekea madhara makubwa mno. Na Huu mgodi wa Fletcher wenyewe ulikuwa unafanya kazi/unatumika.

Ikamsababishia Fletcher hasara ya £937 (Pounds)

Fletcher akayafukuta (pump) maji yatoke nje, lakini tarehe 17 April 1861, pampu yake ilipasuka, na mgodi kwa mara nyingine ukaanza kufurika maji. Kufikia hatua hii, mkaguzi wa migodi aliletwa, wakagundua kuwa, kuna mashimo ya makaa ya mawe yako chini. (Kwa hiyo, Wakawa wamejua chanzo cha yale maji na yalikotokea)!

Tarehe 4 November 1861, Fletcher akafungua kesi ya madai dhidi ya Rylands na mmiliki wa kiwanja, Jehu Horrocks.

JUDGEMENT (HUKUMU).

Kesi ilisikilizwa mara ya kwanza Liverpool Assizes, mwezi wa tisa, mwaka 1862 na Mellor J, Mlalamikaji/plaintiff akashinda kesi huko Liverpool Assizes.

Mahakama ikasema Mshitakiwa (Reyland) alikuwa anawajibika kutokana na ADHA au MADHARA yaliyotokea. Uamuzi ambao baadae ulikuja kupigiliwa Msumari wa mwisho (kuthibitishwa) na Mahakama ya juu kuliko zote Uingereza (House of Lords) kama tutakavyoona huko mbeleni.

Baadae kesi ikaenda sehemu inaitwa Exchequer of Pleas, ambapo ilisikilizwa kati ya tarehe 3 na tarehe 5 May 1865.

Hapa kulikuwa na maswala makuu mawili ya kuamua;
(i) Je! washitakiwa wanaweza kuwajibika kwa makosa ya wakandarasi (Mafundi)?

(ii) Je! washitakiwa wataweza kuwajibika kwa madhara yaliyotokea, hata kama hawakujua na hakuna uzembe wowote waliofanya?

Kwa swala la kwanza, iliamuliwa kuwa hawawezi kuwajibika. Majaji wawili (Pollock CB na Martin B) waliamua kuwa, washitakiwa hawawezi kuwajibika kwa kosa la uzembe (negligence).

Jaji mwingine (Channell B) akajitoa.

Lakini Jaji mwingine (Bramwell B), akakinzana na wenzake na kuamua kwamba, mlalamikaji alikuwa na haki ya kufurahia ardhi/eneo lake, kwa uhuru bila kusumbuliwa (kubugudhiwa) na maji, na kwa hiyo washitakiwa wana hatia ya kuingia kwenye ardhi ya mwingine bila ridhaa yake (trespass) na kusababisha ADHA/KERO (NUISANCE)

Akaongeza kwamba "wanatakiwa kuwajibika, kwa sababu wamesababisha maji kutiririka na kuingia kwenye migodi ya Fletcher, ambapo, kama sio wao hayo maji yasingefika pale."

Fletcher "akakata rufaa" kwenda Exchequer Chamber yenye Majaji sita. Uamuzi wa mwanzo ukapinduliwa (ukatenguliwa) on his favour. (akashinda kesi).

Blackburn J, akiongea kwa niaba ya Majaji wote, alisema; “We think that the true rule of law is, that the person who for his own purposes brings on his land and collects and keeps there anything likely to do mischief if it escapes, must keep it at his peril, and, if he does not do so, is prima facie answerable for all the damage which is the natural consequence of its escape. He can excuse himself by showing that the escape was owing to the Plaintiff’s default; or perhaps, that the escape was the consequence of vis major, or the act of God; but as nothing of this sort exists here, it is unnecessary to inquire what excuse would be sufficient.”

Kiswahili: “Tunafikri kwamba, kanuni ya kweli ya sheria ni kwamba, mtu ambaye kwa malengo yake binafsi analeta kwenye ardhi/eneo lake, na anakusanya na kuhifadhi hapo kitu chochote chenye mwelekeo wa kusababisha SHIDA/ADHA (madhara) pale inapotokea kimehama, sharti akihifadhi kwa hatari (gharama) yake mwenyewe, na kama hafanyi hivyo, anawajibika moja kwa moja kwa madhara yote ambayo asili yake ni matokeo ya kuhama kwa hicho kitu.

Anaweza kujitetea kwa kuonesha kuwa kuhama kwa hicho kitu, kumepelekewa na mlalamikaji kupuuza au kushindwa kutekeleza wajibu wake. Au pengine, kwamba, kuhama huko kulikuwa ni matokeo ya janga la asili au Kitendo cha Mungu. Lakini kwa kuwa hivyo vyote havipo (havikuwepo) hata kimoja kwenye hii kesi. Hakuna haja au umuhimu wa kuuliza utetezi (excuse/defence) gani itakuwa na mashiko.”

Rylands (aliyeshtakiwa akakata Rufaa), kwenda House of Lords. House of Lords, wakatupilia mbali rufaa yake. (The House of Lords dismissed the appeal)

Lord Cairns, akiongea kwa niaba ya House of Lords, alieleza kukubaliana kwao na kanuni iliyotajwa hapo juu na Justice Blackburn.

Hiyo kanuni ndio inaitwa STRICT LIABILITY (maana ya strict liability nilishaeleza kule mwanzoni).

VIGEZO AU MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNATAKA UFAULU KUMSHTAKI MTU KWA KUKULETEA KERO.

(To succeed in this tort, the claimant must show/prove that):

1. The defendant brought something onto his land (kwanza uthibitishe kamba mshtakiwa alileta kitu fulani kwenye eneo lake).

Kisheria, kuna tofauti kati ya vitu vinavyokua venyewe (kwa asili) juu ya ardhi mfano miamba na vile vinavyoletwa au kutengenezwa pale na mtu (defendant) mwenyewe. Kwenye hii kesi (Rylands v Fletcher), yale maji yaliletwa na mtuhumiwa (mshitakiwa) mwenyewe.

2. Non-natural use of the land. Uthibitishe kuwa mshtakiwa aliitumia ardhi kinyume na matumizi ya asili. Kipindi hicho, hapakuwepo na maana kamili ya non natural use of land. Ilitegemeana na mazingira ya kesi husika.

Akitofautisha kati ya natural use na non natural use of land, Lord Cairns alisema ni lazima ithibitike kuwa mlalamikiwa au mshtakiwa alileta kwa makusudi kitu cha hatari kwenye ardhi au eneo lake.

Mfano soma kesi zifuatazo;

-Giles v Walker.
Held: Kwenye hii kesi, Mahakama ilisema mtu hawezi kuwajibika kwa sababu ya miti, vichaka na mimea mingine ambayo imeota kwa asili tu kwenye ardhi yake, hata kama sehemu ya vitu hivyo itachepuka na kuingia kwenye eneo la mwingine.

-Pontordawe RDC v Moore-Gwyn.
Facts: Kwenye hii kesi miamba ilianguka kwenye eneo la mlalamikaji kutokana na hali ya hewa (dhoruba).

Held: Mahakama ikasema miamba haikuletwa pale makusudi kwa hiyo mshtakiwa hawezi kuwajibika).

-Kesi nyingine ni Rickards v Lothian:
Held: “Sio kila matumizi ya ardhi ni non natural use of land. Ila matumizi hayo lazima yawe maalum yanayoambatana na kuongeza hatari kwa wengine, na sio tu matumizi ya kawaida ya ardhi, au isiwe matumizi ambayo ni sahihi kwa manufaaa ya jumla ya jamii.”

-Kwenye kesi ya British Celanese Ltd v A H Hunt Ltd, Mahakama iliamua kwamba matumizi ya ardhi kwenye mali ya kiwanda kwa ajili ya mahitaji ya kiwanda, ni matumizi ya kawaida ya ardhi.

-Kwenye kesi ya Cambridge Water v Eastern Counties Leather, Mahakama ilisema kuhifadhi kiwango kingi cha kemikali kwenye mazingira ya kiwandani, itachukuliwa kuwa ni aina ya matumizi ya ardhi yasiyo ya asili.

Mwisho, suala hili lilipata ufumbuzi kwenye kesi ya Transco ambapo, Lord Bingham aliweka bayana kwamba, matumizi yasiyo ya asili ni pale ambapo mtu anatumia kupita kiasi (extraordinary) na isivyo kawaida (unusual).

Kwa hiyo ‘non natural use of land’ ni kuleta au kuweka kwenye ardhi kitu fulani ambacho ardhi kwa hali yake ya asili isingeweza kuwa nacho. Na kitu hicho lazima kiwe ambacho kikitumiwa kwa matumizi maalum kinaongeza hatari kwa wengine.

Hata hivyo, non natural use of land haihusu kila matumizi yoyote ya kawaida ya ardhi. Mfano kutiririka kawaida kwa maji. Isipokuwa, utawajibika tu kwa kuendesha ovyo shughuli halali lakini ambayo, kutokana na jinsi ilivyo na mazingira yake, sio ya kawaida, imepita kiasi au sio sahihi.

Soma pia kesi za:

-Ellison v Ministry of Defence (1997).
-Read v Lyons [1947]

3. Jambo la tatu, unatakiwa uthibitishe kwamba hicho kitu kilicholetwa hapo ardhini kina mwelekeo wa kuleta au kusababisha madhara ikitokea kimehama. (The thing brought onto the land must be something likely to do mischief if it escapes)

4: Escape. Lazima hicho kitu chenye mwelekeo wa kuleta madhara kiwe kimehama au kilihama kutoka eneo kilipo na kuleta madhara. (The thing did escape and cause damage).

5: Foreseeability. Hayo madhara yawe yalikuwa yanaonekana. Soma Cambridge Water Case (1994).

REMEDIES/NAFUU ZILIZOPO.
-Utalipwa fidia (damages).

DEFENCES TO THE RULE IN RYLANDS V. FLETCHER (UTETEZI AU HOJA ZA KUJITETEA).

Kuna mazingira ambayo kanuni ya strict liability kwenye hii kesi haiwezi ikafaulu kukufunga au kukutia hatiani.

Unaweza kujitetea kwa kutoa hoja zifuatazo.

1: CONSENT (RIDHAA) volenti non fit injuria. Kama mlalamikaji mwenyewe, kwa kutamka au kwa vitendo/viashiria, aliridhia uwepo wa hicho kitu ambacho ni chanzo cha hatari husika, na ukute hakuna uzembe kwa upande wako. Soma kesi ya Kiddle v City Business Premises Ltd

2: COMMON BENEFIT (MANUFAA YA PAMOJA).
Kama chanzo cha madhara kiliachwa hapo kwa manufaa ya pande zote mbili (mlalamikaji na mlalamikiwa), basi mshtakiwa hatakuwa na hatia kikihama na kuleta hasara. Inaelekea kufanana ni ile ya juu (ridhaa). According to Winfield & Jolowicz, “common benefit seems redundant (and indeed misleading) as an independent defence”
Soma kesi ya Cambridge Water Co. v Eastern Counties Leather, (1994)

3: ACT OF STRANGER (KITENDO CHA MPITAJI AU MGENI).
Ikiwa madhara yamesababishwa na mpitaji au mgeni ambaye alikuwa nje ya uwezo wako, hapo pia hautawajibika. Soma kesi ya Rickards v Lothian [1913].

Ila kama kitendo cha huyo mgeni au mpitaji kinaweza kuonekana mapema na madhara yakazuilika, basi una wajibu wa kuwa mwangalifu kuzui madhara yasitokee.

4: STATUTORY AUTHORITY (MAMLAKA KISHERIA): Sheria inaweza kumtaka mtu au kampuni kufanya shughuli fulani. Hapo mlalamikiwa hatawajibika. Soma kesi ya Green vs. Chelsea Waterworks Co. (1894).

5: ACT OF GOD (TUKIO LA KIMUNGU).
Haya ni matukio ambayo hakuna binadamu anaweza kuyatabiri kabla hayajatokea, hata ajibidishe vipi. Ni matukio yaliyo nje ya uwezo wa mwanadamu. Mfano wa Act of God huwa ni matukio kama Sunami, kimbunga, tetemeko la ardhi n.k Soma kesi zifuatazo
-Greenock Corp v Caledonian Railway.
-Tennent v Earl of Glasgow (1864).
-Nichols v Marsland (1876).

6: DEFAULT OF THE CLAIMANT (MAKOSA YA MLALAMIKAJI MWENYEWE).
Kama madhara yametokana na makosa ya mlalamikaji mwenyewe (contributory negligence), hakutakuwa na kuwajibika.

Imeandaliwa na kuletwa kwako na Zakaria (lawyer by profession)
WhatsApp: 07-54575246.
 
Haya ni matukio ambayo hakuna binadamu anaweza kuyayabiri kabla hata ajibidishe vipi. Ni matukio yaliyo nje ya uwezo wa mwanadamu. Mfano wa Act of God huwa ni matukio kama Sunami, kimbunga, tetemeko la ardhi n.k Soma kesi zifuatazo
-Greenock Corp v Caledonian Railway.
-Tennent v Earl of Glasgow (1864).
-Nichols v Marsland (1876).

6: DEFAULT OF THE CLAIMANT (MAKOSA YA MLALAMIKAJI MWENYEWE).
Kama madhara yametokana na makosa ya mlalamikaji mwenyewe (contributory negligence), hakutakuwa na kuwajibika.

Imeandaliwa na kuletwa kwako na mimi Zakaria (lawyer by profession)
WhatsApp: 07-54575246.
zakariaemmanuelzakaria@gmail.com
Mada nzuri sana ila nimesoma na ku-note baadhi ya mambo ambayo umenitatiza, mawili yakiwa ni yafuatayo ulipokuwa unaongelea conditions za mtu ku-qualify for STRICT LIABILITY na hivyo kupelekea kupeleka kesi mahakamani. Ukiangalia kwenye kesi ya hwa wawili uliowatolea mfano hapa, mimi niwaite A Vs B;
Kwenye kipengele cha cga pili kinachosema:

Non-natural use of the land. Uthibitishe kuwa mshtakiwa aliitumia ardhi kinyume na matumizi ya asili.
Hii hoja hapa inanitatiza ukizingatia kesi hii ilivyokuwa kwa sababu kuchimba bwawa siyo ILLEGAL na wala hakukuwa ILLEGAL; na hivyo matumizi ya ardhi hayakukiukwa kwa namna yoyote ile; yaani ardhi haikutumika kinyume cha sheria bali ilitumika kama inavyotakiwa. HIYO MOJA

PILI: Umeandika hivi:
Akitofautisha kati ya natural use na non natural use of land, Lord Cairns alisema ni lazima ithibitike kuwa mlalamikiwa au mshtakiwa alileta kwa makusudi kitu cha hatari kwenye ardhi au eneo lake.

Bwawa siyo kitu cha hatari; uhatari wa bwawa unakujaje hapa?

Labda ukiniambia kuwa labda
"mshtakiwa alisababisha uwepo wa mchakato ambao ni LEGAL lakini ambao kwa bahati mbaya uliambatana na kitu kingine cha hatari, na pasipo yeye mshitakiwa kuwa amejua hatari iliyokuwa imeambatana na mchakato huo; kabla na baada ya mchakato huo,...."

Ukisema hivyo, hapo ndiyo naweza kuelewa, ukizingatia kesi iuliyoileta hapa

Somo la sheria nalipenda sana ila sikubahatika kulisoma kwa kiwango nilichokihitaji
 
Unaweza kujitetea kwa kutoa hoja zifuatazo.

1: CONSENT (RIDHAA) volenti non fit injuria. Kama mlalamikaji mwenyewe, kwa kutamka au kwa vitendo/viashiria, aliridhia uwepo wa hicho kitu ambacho ni chanzo cha hatari husika, na ukute hakuna uzembe kwa upande wako. Soma kesi ya Kiddle v City Business Premises Ltd

2: COMMON BENEFIT (MANUFAA YA PAMOJA).
Kama chanzo cha madhara kiliachwa hapo kwa manufaa ya pande zote mbili (mlalamikaji na mlalamikiwa), basi mshtakiwa hatakuwa na hatia kikihama na kuleta hasara. Inaelekea kufanana ni ile ya juu (ridhaa). According to Winfield & Jolowicz, “common benefit seems redundant (and indeed misleading) as an independent defence”
Soma kesi ya Cambridge Water Co. v Eastern Counties Leather, (1994)

3: ACT OF STRANGER (KITENDO CHA MPITAJI AU MGENI).
Ikiwa madhara yamesababishwa na mpitaji au mgeni ambaye alikuwa nje ya uwezo wako, hapo pia hautawajibika. Soma kesi ya Rickards v Lothian [1913].

Ila kama kitendo cha huyo mgeni au mpitaji kinaweza kuonekana mapema na madhara yakazuilika, basi una wajibu wa kuwa mwangalifu kuzui madhara yasitokee.

4: STATUTORY AUTHORITY (MAMLAKA KISHERIA): Sheria inaweza kumtaka mtu au kampuni kufanya shughuli fulani. Hapo mlalamikiwa hatawajibika. Soma kesi ya Green vs. Chelsea Waterworks Co. (1894).

5: ACT OF GOD (TUKIO LA KIMUNGU).
Haya ni matukio ambayo hakuna binadamu anaweza kuyayabiri kabla hata ajibidishe vipi. Ni matukio yaliyo nje ya uwezo wa mwanadamu. Mfano wa Act of God huwa ni matukio kama Sunami, kimbunga, tetemeko la ardhi n.k Soma kesi zifuatazo
-Greenock Corp v Caledonian Railway.
-Tennent v Earl of Glasgow (1864).
-Nichols v Marsland (1876).

6: DEFAULT OF THE CLAIMANT (MAKOSA YA MLALAMIKAJI MWENYEWE).
Kama madhara yametokana na makosa ya mlalamikaji mwenyewe (contributory negligence), hakutakuwa na kuwajibika.

Imeandaliwa na kuletwa kwako na mimi Zakaria (lawyer by profession)

6: DEFAULT OF THE CLAIMANT (MAKOSA YA MLALAMIKAJI MWENYEWE).
Kama madhara yametokana na makosa ya mlalamikaji mwenyewe (contributory negligence), hakutakuwa na kuwajibika.

Imeandaliwa na kuletwa kwako na mimi Zakaria (lawyer by profession)
WhatsApp: 07-54575246.
zakariaemmanuelzakaria@gmail.com
Hizi hapa zinashahibiana kidogo na zile za kwenye LAW OF AGENCY; AGENCY BY NECESSITY
Kuna kesi moja siikumbuki ni ya akina nani; agent alikuwa anasafirsisha ngozi kwa njia ya bahari halafu kabla hajazifikisha kule zilikokuwa zinaelekea, ikaonekana kuwa kuna vita ilikuwa tayar imelipuka huko.
Kutkana na vita hiyo kwa faida ya mwenye ngozi, agent aliamua kuziuza ngozi kwa sababu kule alikokuwa anazipeleka palikuwa hapafikiki kutokana na vita iliyokuwa inaendelea
--Agent hakumtaarifu mmiliki wa ngozi kabla ya kuziuza ngozi hizo
--Baada ya kuziuza ndiyo alimtaarifu, ikiwa ni pamoja na sababu iliyopelekea aziuze
--Mmiliki wa ngozi alienda mahakamani na kumshitaki agent
--Agent alishindwa kesi kwa sababu kuu mbili
MOJA: Hakumtaarifu mmiliki wa ngozi kabla hajaziuza
PILI: Pamoja na uwepo wa vita, ilikuwa ni vigumu kwa ngozi hizo kuharibika kama zingeachwa kuuzwa na badala yake kuhifadhiw mahali vizuri.......

I like sheria anyway
 
Back
Top Bottom