Kesi kutekwa MO Dewji yaahirishwa mpaka Januari 21

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,804
4,475
1578399917335.png

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo kwenda likizo.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Chaungu alisema kesi hiyo itatajwa Januari 21, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu.
Watuhumiwa wengine ambao upande wa mashtaka inawatafuta ni raia wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini, wanaodaiwa kumteka bilionea huyo.

Washtakiwa hao ambao hawajakamatwa ni Phila Tshabalala raia wa Afrika Kusini, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior wote raia wa Msumbiji.

Katika kesi hiyo inadaiwa Mei Mosi na Oktoba 10, 2018, katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na Johannesburg Afrika Kusini, kwa makusudi washtakiwa wote kwa pamoja waliendesha genge la uhalifu.

Pia inadaiwa Oktoba 11, mwaka juzi maeneo Hoteli ya Colloseum wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Twaleb pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara MO kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari.

Kadhalika, inadaiwa Julai 10, mwaka juzi maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb alitakatisha fedha ambazo ni Sh. 8,000,000 wakati akijua fedha hizo ni kosa la kushiriki genge la uhalifu na makosa ya kupanga.

MO alitekwa nyara Oktoba 11, mwaka juzi alfajiri maeneo ya Hoteli ya Colloseum wakati akienda kufanya mazoezi na alipatikana Oktoba 20, mwaka huo huo katika eneo la Gymkhana.

Chanzo: Nipashe
 
Huyo mshitakiwa Twaleb ana jina moja tu au wasomaji wote wanamfahamu?
 
Back
Top Bottom