Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
Ahsanteni sana ndugu zangu kwa uvumilivu wenu, kazi mliyonituma niliifanya kama mlivyotaka. Nauli zenu mlizochanga hazikupotea abadani, bali nilisafiri nchi za mbali kumtafuta mtabiri mliyeniagiza kwake.
Mtabiri ametabiri mengi ya kesho yetu, mlisema mnataka kujua kesho yetu ipoje, basi kaeni kitako niwahadithie. Mtabiri alianza kwa kulia maana aliyoyaona kesho hayafai hata kusimuliwa.
Kesho yetu imebeba laana sana, kiasi kwamba Mungu anakasirika kwa matendo ya viumbe alivyoviumba yeye mwenyewe. Mtabiri alisema kwamba, kesho yetu pasi hazitakuwa na maana, kwani mavazi yenye marinda hayatakuwepo kabisa. Kasema si wanawake wala si wanaume wote watakuwa tu kama samaki watadai haki ya kuliwa pande zote mbili.
Mtabiri akasema kwamba kesho yetu imejaa single mama wa kutosha, wale mabinti wote wa leo hii mnaowaona wanalilia haki sawa ili hali hawawezi kuwaheshimu waume zao, basi kesho watabaki kuwalilia vijana wadogo wawe nao kimahusiano na ndio hao hao mashangazi watakaosifika kulea na kuhudumia.
Mtabiri hakuishia hapo tu, aliendelea na kusema kwamba kesho yetu ndoa nyingi zitafungwa bar na mahari itakuwa kreti za bia. Sio tu mioyo itakayoumia sababu ya mapenzi, bali hata maini sababu ya mkojo wa firauni.
Mtabiri akasema kwamba, kesho yetu imejaa matajiri wengi wenye hatia na wasomi maskini wa kutupwa, huku vijana wadogo wakisimama shuleni na kuimba "Elimu ni ufunguo wa maisha"
Mtabiri alisema kwamba kesho yetu ni ya ajabu sana, inanuka dhambi na katu haina hata tone la baraka. Kesho yetu binti wa miaka sita hutaweza kumdanganya chochote kuhusu ngono, sababu utandawazi umemfungua macho kabla ya umri wake wa wazi, na kwa bahati mbaya wazazi hawakumsaidia kwenye malezi.
Kesho yetu imejaa wachungaji wa hovyo, wahuni na wapumbavu wa utotoni ndio watasimama hadharani na kusema ni manabii wa Mungu wa mbinguni. Dini zitachafuliwa, pesa itatawala dunia na mapenzi ndio yatakuwa kipaumbele.
Kesho yetu binadamu watazikwa wakiwa wapungufu wa viungo, maana si tu vidole gumba huko Zimbabwe bali hata macho huko Karambwe watu watauza.
Ile heshima mliyozaliwa mkaikuta haitakuwepo tena, itaishia tu Chalinze bali mjini mama mkwe na mkwe wake watalala kitanda kimoja na ku share shuka moja, wenyewe wakiita ni uzungu.
Ndugu zangu kesho yetu ni mbaya sana, kesho yetu pesa ndio itakuwa Mungu, yaani watu watadiriki kuisujudia bila hata kumkumbuka aliewaleta kwenye dunia. Dhambi zitapimwa kwa kilo, magonjwa yatasambazwa kwa lita na uaminifu utapimwa kwa fedha.
Kesho yetu ni ya hovyo sana, vijana waliokosa malezi ya wazazi wao, wakakosa elimu shuleni kwao, wakakosa tumaini mioyoni mwao, wakakosa hofu kwa Mungu wao ndio hao hao watataka vyeo kuongoza taifa lao. Hebu fikiri tutakuwa na taifa la aina gani ??
Inasikitisha ndugu zangu, mtabiri akaendelea na kusema kwamba (itaendelea 74%)
Amani Dimile 
#keshoyetu #amanidimile #mwana_ukae #fikrazadimile #misemo_ya_hekima #mtabiri #vijana #vijanawahovyo #taifalahovyo
Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app