Kesho ni zamu ya Profesa Mwesiga Baregu

Kesho ni zamu ya Profesa Mwesiga Baregu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Kesho kutakuwa na Kongamano la Katiba mpya kujadili changamoto zinazoukabili mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya hapa Tanzania. Kongamano hili litakalorushwa moja kwa moja na ITV, litafanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza-Dar es Salaam.

Watoa mada katika Kongamano hilo watakuwa waliokuwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba, Profesa Mwesiga Baregu na Ndugu Awadh Ali Said. Kesho itakuwa ni zamu ya Wajumbe hawa wa zamani wa Tume kusema 'neno' juu ya Maoni ya Wananchi wa Tanzania waliyoyatoa na kuwekwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa katika Bunge Malum la Katiba.

Tayari,walishajitokeza mara kadhaa Wajumbe wengineo wa Tume ya Katiba na kutetea bila kupepesa macho maoni hayo ya wananchi. Wa kwanza ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba.Jaji Warioba alifuatiwa na Prof.Palamagamba J.A.M.Kabudi na Ndugu Humphrey Polepole.

Mjadala unaendelea na wananchi wote mnakaribishwa.....
 
CCM haipendi kabisa hii kitu - ni mwiba kwao.
 
Najua ccm hawataki lakini taratibu dozi itawaingia.....ila ni vichwa vigumu sana.
 
natumai na radio ya wananchi radio one itakuwa hewani hata wale wasio na umeme kule kwetu dabia wapate ilimu muhimu
 
Waendelee kuwasha moto, ili wananchi wapate katiba yao, walioitolea maoni yao, Thats all
 
Kesho kutakuwa na Kongamano la Katiba mpya kujadili changamoto zinazoukabili mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya hapa Tanzania. Kongamano hili litakalorushwa moja kwa moja na ITV, litafanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza-Dar es Salaam.

Watoa mada katika Kongamano hilo watakuwa waliokuwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba, Profesa Mwesiga Baregu na Ndugu Awadh Ali Said. Kesho itakuwa ni zamu ya Wajumbe hawa wa zamani wa Tume kusema 'neno' juu ya Maoni ya Wananchi wa Tanzania waliyoyatoa na kuwekwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa katika Bunge Malum la Katiba.

Tayari,walishajitokeza mara kadhaa Wajumbe wengineo wa Tume ya Katiba na kutetea bila kupepesa macho maoni hayo ya wananchi. Wa kwanza ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba.Jaji Warioba alifuatiwa na Prof.Palamagamba J.A.M.Kabudi na Ndugu Humphrey Polepole.

Mjadala unaendelea na wananchi wote mnakaribishwa.....

Kesho Jumamosi au Jumapili? Kuna uzi humu ulisema ni J2, tunapmba usahihi wa siku! Kuhusu muda nadhan ufafanuz uko sawa!
 
Tumechoka na hii mikatiba yao tunataka katiba ya zamani iendelee mambo ya kupiga kelele wapate kula tumechoka wasituzoee kabisa watanzania tunataka mambo ya msingi siyo katiba.
 
Back
Top Bottom