germve
Senior Member
- Jul 22, 2017
- 126
- 132
WAKATI NA MAISHA
Time will tell! Huu ni msemo maarufu wa kizungu wenye dhima ya kutukumbusha umuhimu wa matumizi mazuri ya muda.
Hakuna asiyejua kuwa kwenye maisha kuna kipindi cha neema na kipindi cha dhiki (changamoto). Kama ile simulizi ya miaka saba ya neema na ile miaka saba ya njaa tunayoisoma kwenye biblia.
Kuna kipindi cha faida kubwa na kuna kipindi cha hasara kubwa, bila kujali ni biashara ya kuuza dagaa ama ya kuuza magari, lakini kuna hakika ya upepo mzuri katika mwenendo wa chochote unachokifanya katika wakati fulani.
Uhakika huu hufuatiwa na kipindi cha upepo mbaya na mambo kwenda mrama.
Kuna wakati mambo yanaweza kukunyokea mpaka ukashangaa. Na kuna kipindi changamoto zinaweza kukuandama mpaka ukadhani umelogwa.
Kuna wakati fulani unaweza kuwa kwenye upepo mzuri kifedha kiasi kwamba shilingi laki tano ukaweza kuzitumia kwa siku mbili tu katika anasa na matanuzi mengine yasiyo ya msingi, lakini kuna nyakati zitakuja utaitafuta na kuisubiri laki tatu kwa usongo na shauku kuliko walinzi wanavyoingoja asubuhi.
Kuna wakati fulani umbo lako, siha na afya vinaweza kukupa jeuri ya kufanya UFUSKA bila kujali chochote, ikiwemo kumkosea Mungu na pia kupata magonjwa kama UKIMWI, lakini kuna nyakati utalia na kujuta peke yako hususani kile kipindi utakapoambiwa ini lako halina tena uwezo wa kupambana na makali ya dawa za ARV, kipindi ambacho jeuri ya kufanya umalaya kwa kutegemea madawa ya hospitalini itakapokuwa imefikia ukingoni.
Kuna nyakati unaweza kukosa kuona thamani ya kazi yako, mwenzi wako, mke, mme au mpenzi wako na kumuona boya, lakini kuna nyakati zitakuja ukiwa umekutana na kanyaboya halisi, utaikumbuka thamani halisi ya kile ulichopuuza awali.
RAI
Tujifunze kupanda mbegu njema katika nyakati za heri ili zikija nyakati ngumu tuweze kuvuna yale mema tuliyoyapanda na yatusaidia kuishi kwa heri katika nyakati ngumu zenye changamoto.
germve himself