Kesho naitupa line ya Halotel rasmi

Hawa wahuni wa halotel wafanyiwe ukaguzi na TCRA

Haiwezekan mb za buku zinayeyuka kwa muda mfupi ivi

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Mi nishaitupa siku nyingi...maana wezi hawa...alafu modem zao haziko compatible Na windows 10..sasa ya nini kuwa nao....
 
hamieni 4G, hakuna mtandao wa 4G ambao upo slow. vodacom, TTCL, Tigo, smile na smart wote wana 4G fanya utafiti kwako upi una coverage na speed nzuri then nunua. Hata kama network ya 4G ni ndogo itakuwa na speed nzuri tu.
 
Hii 4G mbona tuaisikia tu kwa wengine sisi Geita Iwe vda ni 3G airtel wao ni 2G Halotel labda ununue line ya mwanachuo mbona kuna ubaguzi sana Mjini na vijijini yaani mikoa ya pwani na huku bars mikoa yetu ni kama vijijini tu na ndiko anakotoka munakaya.
 
Kwahiyo TTCL ndio wana coverage kubwa mkuu?fanya utafiti kwanza kuhusu TTCL kabla ya kutupa hiyo line,mtandao wa Halotel una boa sana hasa kwa sasa ambapo umekuwa very slow ukilinganisha na mwanzoni walipoanza ila kwa TTCL nina mashaka unaweza kuichoma moto hiyo line kwani bado hawako vizuri kivile,hawa wana mikakati mizuri sana ila bado tuwape muda wajipange.
 
Mtandao aminifu kwa wateja wake ni airtel. Mtandao wenye coverage nzuri kwa internet ni vodacom. Mtandao wenye coverage nzuri ya kupiga cm hasa kwa cm ndogo ni halotel. Mitandao sumbufu kwa wateja ni karibu zote zinasumbua isipokuwa airtel kidogo wanajitahidi sana ingawa wana minara michache alafu ziko mbali mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…