Salvatory Mkami
Senior Member
- Apr 17, 2013
- 146
- 244
Kwa wale mtakaopata muda siku ya kesho msiache kufuatilia vikao vya Bunge ambapo kambi rasmi ya upinzani Bungeni itasoma bajeti mbadala ya wizara ya fedha kwa mwaka 2017/2018.
Kwa wale wasiotambua au kusahau niwakumbushe tu kwamba kilichosomwa na waziri wa fedha Dk. Mpango ni "Bajeti Pendekezwa" Bunge ndilo hupitisha Bajeti. Kwahiyo tunapaswa kuisikiliza kwa makini "Bajeti Pendekezwa" ya upande wa pili (Upinzani) ili kuona kama kuna mambo muhimu ambayo yanaweza kuiboresha bajeti hiyo ya Dk Mpango, ila tu ninaamini hilo linawezekana iwapo tuna watu wanaojitambua na kukubali kushauriwa kwa maslahi mapana ya taifa!
Natumai kama ilivyo kawaida Kambi rasmi ya upinzani Bungeni itapongeza bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 pale inapotakiwa kupongezwa na kuikosoa pale inapohitaji kukosolewa. Kwa wale vijana wa Lumumba waliozoea kushabikia na kupongeza kila jambo hususani maamuzi na ripoti ambazo hazitakiwi kukosolewa waendelee kushabikia tamthilia namba2 ya mchanga lakini wasisahau kwamba nyeupe haiwezi kuitwa nyeusi!
Hata hivyo sintashangaa iwapo vyombo mbalimbali vya habari vitaelekezwa zaidi katika kurusha tukio la makabidhiano ya ripoti namba2 ya mchanga kuliko bajeti!