Kero zinazowakabili wananchi jimbo la Lupembe, Njombe

Amo90

Member
May 20, 2020
26
75
CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI JIMBO LA LUPEMBE KWA UJUMLA (KERO)

1. ZAO LA CHAI KUKOSA SOKO LAUHAKIKA

Wakulima wa chai Lupembe wamekosa soko la uhakika la kuuzia majani mabichi ya chai. Viwanda vya chai vilivyopo vya Ikanga na Lupembe vinapokea majani mabichi ya chai lakini haviwalipi wakulima. Mfano hadi sasa wakulima wanadai zaidi ya Tsh. 800,000,000 (Milioni 800) Wakulima wameanza kutelekeza mashamba ya chai kwa sehemu kubwa.

2. KIWANDA CHA CHAI LUPEMBE

Kiwanda cha chai Lupembe kinatakiwa kurudishwa kwa wananchi. Maamuzi haya yalifanywa na mahakama ya rufani tarehe 21/09/2021. Hadi sasa amri hiyo ya mahakama haijatekelezwa kutokana na serikali (MSAJILI WA HAZINA) kushindwa kusimamia zoezi hilo.

3. MIUNDO MBINU MIBOVU YA BARABARA KATIKA MAENEO YA UZALISHAJI CHAI

Hali ya mtandao wa barabara katika maeneo yanayozalisha majani ya chai ni mibovu. Hali hiyo inasababisha majani ya chai kuharibika kutokana na kutosafirishwa kwa wakati hasa katika kipindi cha mvua nyingi.

4. MRADI WA AGRICON-BORESHA CHAI

Kuna mradi unaoitwa AGRICON-BORESHA CHAI unaofadhiliwa na jumuiya ya ulaya katika nyanda za juu kusini. Lupembe ilipewa fedha za kujenga barabara za chai kilomita 59 kwa kiwango cha lami tangu mwaka 2020. Hadi sasa kazi hiyo haijafanyika. Wilaya ya Mufindi na Rungwe kazi hiyo imekamilika. Tunashindwa kuelewa kwa nini Lupembe tunabaguliwa.


5. PEMBEJEO ZA RUZUKU

Upatikanaji wa pembejeo za ruzuku ni mgumu sana kwa Lupembe. Ukihitaji kupata pembejeo za kilimo za ruzuku inakulazimu kufuata hadi Njombe mjini. Aidha mbolea aina ya NPK 25-5-5+3S kwa ajili ya zao la chai haipatikani Njombe.

6. KITUO CHA AFYA LUPEMBE

Kituo cha Afya Lupembe kinahitaji ukarabati na kupanuliwa. Pia tunahitaji gari la wagonjwa kwani gari lililopo ni chakavu. Tunahitaji pia kujengewa jengo la kuhifadhia maiti. Tumekuwa tukiahidiwa na viongozi lakini hakuna utekelezaji.

7. BARABARA YA KIBENA – LUPEMBE MADEKE – MLIMBA KATIKA KIWANGO CHA LAMI



UMUHIMU WA BARABARA HII KWA UCHUMI WA TANZANIA

I. Inaunganisha mkoa wa Njombe na Morogoro

II. Inapita katika maeneo ya uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara na chakula

III. Inapita katika maeneo yanayostawisha misitu ya mbao kwa wingi kuliko eneo lolote hapa nchini ukiacha msitu wa serikali wa SAO HILL

IV. Inapita katika maeneo yenye madini ya aina mbalimbali kama dhahabu

V. Inapita kwenye maeneo yenye mabonde na mito kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kama mpunga

VI. Inapita katika ofisi za Halmashauri ya Njombe DC

CCM imeshindwa kuweka kwenye Ilani ya uchaguzi barabara hii katika awamu zote hadi awamu ya tano japo hadi leo hakuna kilomita moja ilikwisha jengwa kwa lami .
 
Mpaka sasa nashindwa kuelewa Njombe inafeli wapi..

Mkoa una miti,mahindi,maji kila sehemu,hali ya hewa safi,na vilimo kibao vinakubali na mara nyingi sio kame inafeli wapi.

Kibena - Lupembe ile barabarani vumbi lake sio mchezo...japo sikuwahi fika huko mbele niliishia mitaa ile ile
 
Tatizo la middle class, hadi leo hajui njombe wanafeli wapi, endeleeni kuchagua chama cha mafisadi, wala pie 🥧 ya taifa ni royal families tu
 
Back
Top Bottom