Kero zangu kuhusu tume ya katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero zangu kuhusu tume ya katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchongameno, Apr 9, 2012.

 1. mchongameno

  mchongameno Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuchukua nafasi hii kutoa maoni yangu kuhusu tume ya mabadiliko ya katiba iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kama ifuatavyo.

  Kwanza ni kuhusu suala la uwiano wa wakilishi kutoka katika pande zote za Muungano. Kwa hakika hata kama ndivyo ilivyoamuliwa tangu awali kwamba Wajumbe wa Tume kuwa idadi sawa kati ya Tanzania bara na Zanzibar ni dhahiri kabisa kuwanyima haki watu wa Tanzania Bara ambao idadi yao ni kubwa mno kuliko Tanzania Visiwani. Tanzania Bara ina watu takribani milioni 42 na Zanziba ina watu milioni 2. Hivyo Si sahihi kabisa uwiano kuwa sawa. Kufanya hivyo ni kuwanyima haki watu wa Tanzania Bara. Pili kama kila siku inasisitizwa kwamba baada ya muungano Zanzibar ilipoteza Utaifa wake Je ni kwa kigezo gani kuwa na idadi sawa. Pia Zanzibar wana Katiba yao ambayo haiigiliwi na watu wa Bara. Sasa ni kwanini Katika katiba hii wawe na uwiano wa Idadi ya wajumbe kwenye katiba inayowahusu Watanzania ikiwa wao idadi yao ni ndogo katika muungano?

  Suala la Pili ambalo kwangu naona ni tatizo ni hili suala la uwiano wa watu kulingana na Imani zao nikimaanisha dini zao. Kumekuwa na malalamiko mengi hasa kutoka kwa waislam kwa miaka mingi kwamba hawatendewi haki na Serikali hasa kutokana na muundo wa katiba yetu tunayoitumia sasa hivi. Katika Tume hii iliyoundwa na Rais idadi ya Waislam ni kubwa mno hivyo kuibua hisia kuwa Rais ana agenda ya Siri ya kuwabeba Waislam. Hili lina maana kubwa kwani hata Muundo wa Serikali yetu unalalamikiwa kuwa umejaza Waislam wengi kuliko Watu wa Imani nyingine.Tanzania si nchi ya kidini lakini tukumbuke kuwa Watanzania ni watu wenye imani tofauti za kidini.

  Suala la tatu ni kuhusu ushiriki wa wajumbe kutoka taasisi mbalimbali kama ilivyoelezwa awali. Pamoja ya kwamba tume imetajwa lakini hakuna ufafanuzi unaoonyesha ushiriki wa wajumbe kutoka Taasisi zao kama tulivoelezwa awali. Ninaongea hivi nikiwa na maana ya kwamba tulielezwa kwamba kutakuwa na wawakilishi kutoka taasisi mablimbali kama Wawakilishi kutoka taasisi za Kisheria, Wanaharakati, Taasisi za kidini, Walemavu, Vyama vya Siasa nk. Lakini katika tume hii hakuna ufafanuzi unaodhihirisha kuwa fulani anawakilisha nini.

  Ni matumaini yangu Maoni yangu hayo machache yatafanyiwa Kazi.

  Asanteni.
   
 2. l

  lubaga Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JAKAYA KIKWETE .Kwanza ututajie ni vigezo gani ametumia kuwateua waislamu wote hao,pili ainishe majukumu ya tume itafanyakazi gani ilitujiridhishe kama uteuzi wake unawiana .huyu yupo kwa ajili ya kutekeleza mpango maalumu wa maazimio ya abuja dhidi ya wakriso.
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo.
  Tunakushukuru JK kwa kuwa umetupa nafasi wazanzibar kuamua nini tunataka!
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hayo mambo si ya kupuuzwa kabisa lazima kuwe na uuwiano
   
 5. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Pole sana!!!.
  :disapointed::disapointed:
   
 6. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  utakuja kuniambia kama mtaamua mnacotaka au CCM - Dodoma inachotaka.
  Wait and see!!
   
Loading...