Niliwahi kuleta uzi hapa kuhusiana na wapiga debe Kahama. Nimefika stendi hii juzi mambo ni sawa kabisa. Hakuna bugudha za wapiga debe na kila kitu kipo shwari. Katika kuulizia kulikoni; nikapata habari kuwa, siku chache zilizopita kulifika ugeni mzito katika stendi hii akiwapo afande RPC wa mkoa na kunyoosha mambo ambapo wabugudha abiria kadhaa waliangukia mikononi mwa Polisi:
Kero za Polisi kwenye Stand za Mabasi TAKUKURU mnafahamu?
Sasa hebu angalieni hili la Nyashishi Mwanza katika hii clip ninayoambatanisha. Hapa wapiga debe wanakomaa kiasi cha kutaka kupiga hata mwakilishi mdau wa usafiri. Angalia tamko la Sumatra na la polisi katika sakata hii. Hakuna lolote kuhusiana na hawa wapiga debe. Indirectly si Polisi wala Sumatra Mwanza inayoonekana kujali wala kuhusika na adha ya wapiga debe hawa. Kwa maana nyingine kwa muonekano huo wapiga debe hawa wapo pale kihalali. Hawa wenye mamlaka, hawaoni hata mahusiano ya nauli hizi wanazojaribu kuongelea na tatizo la wapiga debe hawa ambao wako tayari hata kupigana kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwapo hapo stendi.
Mwanza jifunzeni kwa njia zilizofuatwa kusuluhisha suala la wapiga debe Kahama. Wapiga debe hawa ni kero na chanzo cha usumbufu wote kwa abiria ikiwamo kuwaibia moja kwa moja au indirectly kwa kupitia katika nauli kama ambavyo sasa mnavyodhania kuwa wenye tatizo na hizo nauli ni hao madereva wa daladala. Kumbukeni kuwa wapiga debe hawa wanajipatia mapato kinyemela tokea katika nauli hizo hizo.
Kazi kwenu Mwanza wakati tunapo wapa pongezi Kahama na kuwatakia kheri kuwa hali ya sasa isije legezewa kamba.