Kero Za Wananchi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero Za Wananchi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by vivian, Jun 4, 2012.

 1. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hivi Mods inawezekana Jukwaa La kero za Wananchi kuanzishwa?

  Nina uhakika Jukwaa hili litavuta hisia ya Viongozi wengi hasa wabunge na watazifikisha kunakostahili.
  Hapa Dar es salaam kuna kero nyingi ambazo wananchi tungependa kuwafikishia viongozi wetu na nafikiria hii ndio itakua njia sahihi ya kuwasilisha kero zetu.

  Naomba nianze na kiongozi mchapa kazi mzee Magufuli:
  Mheshimiwa Traffic lights za Changombe na zile za some distance from sabasaba hazifanyi kazi. Nilitegemea kwa tatizo hili tungekuwa na Mbadala wa Askari wa kuongozea magari muda wote. ila la kushangaza ni mara chache sana utakuta askari maeneo yale.

  Hivi mkisikia kuna DCM limepta ajali pale na makumi ya maisha ya watanzania wasio na hatia yamepotea ndio mtachukua hatua? Binafsi ninaamini sana katika uchapa kazi wa magufuli, sitaki kuamini ukakamavu wake ni kwenye majukwaa tu. Ninaaamini na nitabaki kuamini kuwa huyu mmoja kati ya viongozi wa wachapa kazi hapa Tanzania.

  Nina kero nyingi ambazo nataraji kiziwalisha kwenye hilo jukwaa la ''KERO ZA WANANCHI''

  Updates:

  Hii Imetokea leo. tar 6/6/12. marely 2 days after I stated this thread:


  Uzembe Wa Madereva Na Ubovu Wa Taa Barabarani Kusababisha Ajali


  [​IMG]

  [​IMG]


  [​IMG]
  Ajali hii imetokea alfajir ya leo kwenye makutano ya mandela road na kilwa road ilihusisha malori mawili kwenye taa za kuongozea magari uhasibu ambapo mashuhuda walisema lori la kampuni ya Azam halipo pichani, lilishika breki ghafla katikati ya taa za kuongozea kupisha gari ndogo iliyokuwa ikitokea jitegemee kwenda sabasaba,dereva wa lori alishindwa kulidhibiti wakati akijaribu kulikwepa lori la Azam na kuishia kugonga nguzo ya Taa na kuanguka ,dereva alivunjika miguu yote miwili na kukimbizwa hospitalini.


   
 2. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kero ya pili:

  Mashirika mengi NGO's yanaanzishwa kwa lengo la kuwasaidia watanzania lakini kiukweli ajira nyingi wanajipatia wao wenyewe. wanajilipa mishahara mikubwa ambayo hailingani na kzi wanazo zifanya. watanzania walio azjiriwa kwenye nafasi za chini kwa mishahara kiduchu ndio wanaongaika kufanya kazi zilizo ainishwa kwenye proposals.

  Sio hivyo tu. Nafasi nyingi za ajira pia kwenye makapuni mbali mbali zimejazwa na wakenya. Kisa watanzania hatuwezi kujieleza kwa Kiingereza kwenye interviews.

  Sijui waziri wetu husika unalionaje hili?
   
 3. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kero Number Tatu:
  Udhibiti wa madereva wazembe wanaosababisha foleni katika jiji la dar es Salaam.
  Pamoja na miundo mbinu ya jiji ya Dar es salaam kuwa na mapungufu hivyo kusababisha foleni, Asilimi zaidi ya 60 ya foleni husababishwa na Madereva wazembe hasa dala dala kushusha na kupakia abiria katikati ya bara bara. Wengine wapo kwenye vituo lakini bado wanakaidi kuingia kwenye vituo na kupakia abairia nje ya vituo.

  hivi trafic hawatoshi kupangwa kila kituo?
   
 4. Gele vaheke

  Gele vaheke Senior Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana vivian we umenena na jua wakuu wame liona hili watalifanyia kazi
   
 5. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kero Number 4.

  Wananchi tunaburuzwa.
  Hivi karibuni tumesikia mikakati ya mifuko ya Hifadhi ya jamii kutorejeshi michango ya wanachama pindi wanapo fukuzwa au kuacha kazi kwa hiari.

  Tunaomba Ukumbukwe hii michango ndio mwokozi wa mwanachama pindi anapo pata matatizo ya kupoteza kazi yake. Hilo shauri la kurejesha michango pind mwanachama anapofikisha umri wa kustaafu binafsi siliafiki kabisa!!! Bora nikae niuze vitunguu kule kariakoo.

  Hivi m2 una miaka 70 unapewa Milioni 100 ikusaidie nini? Hiyo si inaishi kuwa pocket money tu. Kwa hili wabunge mkiikubali hii sheria mtakua mume tuua kabisa. I will just resign on the spot.
   
Loading...