Siempre Hechos
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 1,231
- 1,538
Uendeshaji bodaboda i umerahisisha usafiri kwa kiasi falni na pia umeajiri vijana wengi na baadhi yao umewapunguzia ukali wa maisha na pia kuachana na vitendo vya uvunjifu wa sheria kama wizi (japo wapo wanaotumia fursa hii kuwa wezi wazuri). Lakini katika ajira yao hii kumekuwa na kero kadha wa kadha hasa wanapokuwa njia kuu kama ifuatvyo japo kwa uchache;
1. Wanaongoza kuvunja sheria za barabarani (kwenye makutano ya barabara na hasa kwenye taa za barabarani wengi hawazieshimu) na kusababisha ajali za makusudi. (Afisa usalama barabarani wanawaangalia tu)
2. Wanaharibu magari ya watu eidha kwa kukwangua rangi au kuvunja kabisa baadhi ya vifaa kama side mirrors na taa hasa pale wanapopita katikati ya magari kwa tahadhari dhaifu wakiwa mwendo mkali.
3. Wanaover-take karibu kabisa mbele ya gari inayotembea bila tahadhari ya kutosha kwamba lolote linaweza kutokea kwamba anaweza kuteleza akasababisha kugongwa na gari.
Serikali tunaomba wawangalie sana hawa watu, wamejipa uhuru na mamlaka makubwa sana ya kufanya watakavyo hata pale wanapokuwa wamekosea wao, ajali inapotokea kati ya gari na boda boda hualikana kwa wingi na kufanya uharibufu kwa upande wa pili kisa tu mwenzao kapata ajali kati yake na mwenye gari. Hili ni bomu, isipochukuliwa kwa umakini mkubwa, vitendo vyao vya uharibifu wanavyofanya vitageuka kuwa uhalifu uliohalalishwa.
Karibuni kwa mjadala.