Kero za Sabasaba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero za Sabasaba!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GreatConqueror, Jul 2, 2009.

 1. GreatConqueror

  GreatConqueror Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wakuu kama mjuavyo wikiend ilyopita maonyesho ya 'kimataifa' ya Sabasaba yalianza Dar na baadhi yetu nadhani tumebahatika kufika kule, pamoja na maana yake nzuri, maonyesho haya naona yana kasoro/kero kadhaa ila kubwa ambayo naiona na ambayo ni dhahiri ni MAKELELE (sound pullution). Kuna baadhi ya waonyeshaji sijui ni kukosa mbinu mbadala za kuita watazamaji au kukosa mwongozo wa maana ya maonyesho, wanafungulia muziki kwa sauti kubwa sana. Na wengine wamepeleka hadi vikundi vya shoo.

  Ngoma ni pale waonyeshaji wa dizaini hii wanapokuwa karibu karibu, usikivu ni zero. Sasa inakuwa kero kwa waonyeshaji na watazamaji wengine.

  Ikumbukwe kuwa maonyesho haya pia yanakutanisha makampuni ya kibiashara na taasisi/idara za umma ambapo umma unakwenda kupata maelezo ya huduma mbalimbali. Kwa hali hii inakuwa kazi kweli kweli kuelewana. Yaani unaweza kusema afadhali ya Kariakoo kidogo kwa sababu hakuna vumbi.

  BET hili la makelele nalo linahitaji resources?

  Nawasilisha!
   
Loading...