Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,320
- 18,595
Mpaka naweka huu uzi yamenikuta na nimeshindwa kuvumilia.
Hi huduma ya simbanking ni hovyo mno kuliko nilivyokua nafikiria, nina visa viwili nitawaambieni.
Kuna siku nilikua nimekwama sana, nikaamua kuhamisha pesa kutoka benki kuleta tigo pesa, ilikua 60,000 TZS, pesa ilikatwa kwenye akaunti ila kwangu haijafika, nikawapigia simu kupitia namba hii 0714 197 700 nikawaeleza wakasema subiri 24hours, baada ya huo muda hakuna kilichotokea, nikapiga tena wakanipiga danadana nikapata hasira sana, niliamua kutafuta pesa kwingine, mpaka waliporudisha hilo 60,000 ni siku saba zilipita.
Kisa kingine kimenitokea juzi, niliamua kulipia bill ya king'amuzi kupitia simbanking, baada ya muda ikaja message hii "DSTV payment of TZS 00000 to 0000000000(namba yangu ya king'amuzi) failed with reason -Request expired 27-12-2017 12:58:27,
kuangalia akaunti pesa wamekata ila haijaenda Dstv, nikawapigia wakasema subiri 24 hours, baada ya 24 hrs nikapiga wakaleta drama zao.
Mpaka hivi ninavyozungumza pesa haijarudi na sijui itarudi lini.
Leo nikaamua kuwapigia kwa namba hii 0755 197 700 walichonijibu hata Sina hamu nao kabisa eti wanasema subiri mpaka Jumanne ya next week, seriously???? Bank kubwa Kama crdb inakua kama chama cha upatu?
Crdb upande wa simbanking mnaboa sana