Kero ya usafiri wa kupitia Loliondo

Kero ya usafiri wa kupitia Loliondo

Tyupa

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
802
Reaction score
657
Ni jambo la ajabu tena kushangaza kulazimisha magari ya Mlandizi via Loliondo. Kama kuna viongozi wa mkoa wa Pwani walipanga magari hayo yapitie Loliondo kwa hakika walikurupuka sana.

Nashangaa walisahauje yapitie Tumbi Hospital, Mwanalugali na kwingineko kama ambavyo walikumbuka yapitie Loliondo pekee. Ni usumbufu wa hali ya juu kulazimisha mabasi yapitie Loliondo pekee badala ya sehemu zote za mji wa Kibaha.

Vingozi waliopanga utaratibu huu walikuwa hawana kazi ya kufanya kwa sababu mji wowote wa mkoa unatakiwa kuwa na town bus kwa ajili ya kuchukua abiria wa pembe zoni na kuwapeleka stendi kuu. Kulazimisha mabasi makubwa yapitie Loliondo pekee ni kero ambayo inahitaji kurekebishwa haraka sana.

Tunawasihi viongozi wahusika wasitishe haraka safari ya kupitia Loliondo ili waokoe mafuta na usumbufu kwa abiria.Abiria wote hulaani kwa nguvu kila siku kutokana na kero hii ya ajabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom