Kero ya Polisi Mbeya na Bajaji

Author

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
1,709
8,007
Wana JF Habari,

Naamini kama wewe ni mkazi wa Mbeya na ni mtumiaji wa usafiri wa bajaji unaweza kuwa umekutana na kero ya kushushwa kwenye bajaji asubuhi ukiwa unaenda kazini au jioni ukiwa unatoka kazini au ukiwa kwenye mizunguko yako ya kila siku.

Hii inatokana na waendesha bajaji hao kukamatwa kamatwa na askari na kuwekwa kwenye gari za polisi kisha kuhitajiwa kulipa faini ambazo hazina maelezo.

Wakati mwingine waendesha bajaji hao hukamatwa na kuwekwa kwenye gari la polisi kisha askari kutumia bajaji zao kuwafukuzia na kuwakamata waendesha bajaji wengine (Hii baadhi ya dereva bajaji wameeleza)..Na baadhi ya bajaji hukamatwa zikiwa zimepaki vijiweni!!!

Nimefanya utafiti kwa baadhi ya waendesha bajaji na wamedai ya kuwa kuna wengine hawana makosa yaani ana leseni halali, amelipia mapato, SUMATRA, bajaji sio mbovu, tairi ni mpya, bajaji ina bima na alikamatwa akiwa amebeba abiria wawili...Hakuelewa kosa lake wala sababu ya kukamatwa na aliambiwa alipe fain!!

Katika kikao kilichofanyika juzi jumanne kati ya umoja wa bajaji na polisi Mbeya moja kati ya maswali muhimu yaliyoulizwa hayakujibiwa kwa uzito na usahihi kuhusu matukio haya.

Wengi wa abiria na waendesha bajaji wamedhani kuwa hii ni njia ya askari kukusanya mapato kwakuwa bajaji ni wengi hivyo ni rahisi kupata mapato mengi kutoka kwao kwani hata askari wanaochukua faini hizo hawana mashine ya EFD!

Mambo ambayo yanatutatiza watumiaji wa usafiri wa bajaji ni;
1.Kwanini madereva hukamtwa na kuwekwa kwenye gari la polisi bila kuambiwa makosa yao?

2.Kwanini askari wanaowakamata hawana mashine za EFD ili kuwaandikia waendesha bajaji makosa yao na kuwapa risiti?

3.Kwanini wanapowakamata madereva bajaji huwapiga wakati wametii sheria bila shuruti?

4.Kwanini abiria tusijulishwe makosa ya bajaji ili kabla ya kupanda tujiridhishe tuepukane na kero za kushushwa barabarani?

Njia rahisi zaidi ya kudhibiti makosa ya bajaji ni kuwaelimisha abiria, sababu bajaji atahofia kukosa abiria hivyo atafanyia kazi makosa yake. Mimi nimekutana na hii kero mara mbili nikiwa nawahi ofisini asubuhi bajaji akanishusha njiani kisa anaogopa askari, hivyo nikaanza kutafuta usafiri mwingine jambo lililopelekea kuchelewa kazini.

Askari wanasema hichi ni kipindi cha mpito na baada ya muda wataacha kuwakamata bajaji!!!,,,Hii inafanya niamini kuwa ni swala la mapato sababu kuna bajaji zaidi ya 4000 Mbeya!,,Mkifikia malengo bajaji wataendelea na kazi hata kama wana makosa!!!!???

Toeni elimu kwa wamiliki,dereva bajaji na abiria...NJIA MNAYOTUMIA SIO SAHIHI

Naomba kuwasilisha....
 
Pole sana mkuu. Ila pamoja na yote hayo uliyoeleza, mambo mawili ni dhahiri kuhusu bajaj jijini Mbeya;
1. Zimekuwa nyingi kiasi kwamba huo wingi peke yake sasa ni kero.
2. Waendesha bajaj wengi ni kama sheria za barabarani haziwahusu!
 
Kuna kamanda wambeya nilimsikia kwene radio jana anasisitiza dereva bajaji wasipandishe abiria kwene kiti cha dereva mana kosa hilo ndo linalowaghalimu sana
 
hapa bongo hamna sehemu nilioona utaratibu mbovu wa bajaj Kama jiji LA Mbeya, yaani bajaji inapiga root Kama daladala na wanapaki kwenye vituo vya daladala

Madereva sasa ndo kituko 98% ni madogo under 17 wameishia darasa LA 5 au form one yaan hajui hata sheria moja ya barabarani
 
hapa bongo hamna sehemu nilioona utaratibu mbovu wa bajaj Kama jiji LA Mbeya, yaani bajaji inapiga root Kama daladala na wanapaki kwenye vituo vya daladala

Madereva sasa ndo kituko 98% ni madogo under 17 wameishia darasa LA 5 au form one yaan hajui hata sheria moja ya barabarani
Well said mkuu, bajaji Mbeya ni janga!!
 
tena hata mkuu wa trafiki hapa mby anasema kuwa "bajaji mbeya kuna mkono wa kisiasa" yaani nayeye amechoka nazo
 
Nadhani watengenezewe mazingira rafiki tu ya usafirishaji, bajaji zimekuwa msaada mkubwa katika urahisishaji wa usafiri maeneo yasiofikika kirahisi,(hasa ukizingatia mbeya wakazi wengi wanaishi pembezoni mwa mji) ambapo mji unatanuka kwa kasi
 
Nadhani watengenezewe mazingira rafiki tu ya usafirishaji, bajaji zimekuwa msaada mkubwa katika urahisishaji wa usafiri maeneo yasiofikika kirahisi,(hasa ukizingatia mbeya wakazi wengi wanaishi pembezoni mwa mji) ambapo mji unatanuka kwa kasi
Wengine wanashauri daladala ziondolewe kwani bajaji zinakidhi mahitaji...zipo zaidi ya 4000 na bei yake ni rahisi.
 
Back
Top Bottom