Haya ni baadhi tu ya matangazo ya Tigo niliyotumiwa ndani ya masaa 24 yaliyopita. Nilishaomba TCRA watuondolee hii shida. Matangazo haya hayana tija yoyote kwa watumiaji wa mtandao huu, na nina mashaka kama bahati nasibu wanazozihamasisha kuna mtu yeyote amewahi kufaidika nayo kama wanavyotaka tuamini. Hii ni namna nyingine ya kuwapotezea wakati wateja wao, rasilmali ambayo ingetumika kwa namna nyingine kulijenga taifa.