Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Binafsi nasikitika sana ninavyozidi kusikia kwamba viongozi wengine wenye mamlaka hawawapi kipaumbele kina mama, ambao ni mama zao, wake zao, binti zao, bibi zao, shangazi zao, dada zao, wanawakosea heshima kwa kuwalaza chini sakafuni ni aibu kubwa sana kwa serikali. Pongezi kwa Mh Raisi kwa kuendelea kuliona hili kila wakati lakini jipu ni pale wasaidizi wake wanaposhindwa kulitekeleza na kutafuta mbinu za kuhakikisha hawa kina mama hawadhalilishwi hivyo
Rais Magufuli ametembelea kwa ghafla wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam, na kujionea hali ya msongamano mkubwa wa wazazi uliosababishwa na uhaba wa vitanda na nafasi finyu katika wodi hiyo. Una maana viongozi wengine hawakuona? wakurugenzi muhimbili wanafanya nini? wizara inafanya nini? watendaji wengine wote wanafanya nini? wana haki za kina mama mko wapi kupigania hili?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea kwa ghafla wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam, na kujionea hali ya msongamano mkubwa wa wazazi uliosababishwa na uhaba wa vitanda na nafasi finyu katika wodi hiyo.
Rais Magufuli aliyekuwa akitoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokwenda kumuona na kumjulia hali Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery Bin Ally, amelazimika kwenda katika wodi hiyo baada ya msafara wake kusimamishwa na kundi la akina mama, waliomtaka kwenda katika wodi ya wazazi ili akajionee jinsi wazazi wanavyokabiliwa na kero mbalimbali ikiwemo ya kulala chini kutokana na kukosa vitanda.
Baada ya kujionea mwenyewe kero ya msongamano na kuzungumza baadhi wazazi waliojifungua, Rais Magufuli amewaahidi wazazi hao kuwa atashughulikia kero alizozishuhudia.
"Nimeiona hali halisi mimi mwenyewe, watu wanapata shida, watu wana mateso, na ndio maana nimeamua kuja kwa makusudi, sikuomba ruhusa ili nijionee hali ilivyo, nimejifunza mengi, ninayabeba na nitajua namna ya kuyatatua" Alisema Rais Magufuli.
Kuna haja ya kujadili kwa mapana sana hili jipu wanajamiii....