Kero ya barabara ya King'ori - Ngarinanyuki - Oldonyosambu

Kero ya barabara ya King'ori - Ngarinanyuki - Oldonyosambu

Iruru

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2014
Posts
1,469
Reaction score
2,901
Naileta hii habari hapa kwa imani kwamba viongozi wa serikali na hasa wizara ya ujenzi na miundo mbinu ni wapenzi wa jf na hulitumia jukwaa hili kupata habari sahihi zisizochakachuliwa.

Barabara tajwa hapo juu (King'ori - Ngarinayuki - Oldonyosambu) ni barabara muhimu inayounganisha mikoa ya Arusha-Kilimanjaro na nchi jirani ya Kenya.

Ni barabara hii ambayo pia huwapeleka watalii katika hifadhi muhimu ya Arusha na mlima Meru. Ni bahati mbaya kwamba pamoja na umuhimu wa kiuchumi iliyonao kwa wananchi wa maeneo tajwa na Tanzania kwa ujumla, haijawahi kupewa kipaumbele kwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Hii ni barabara kongwe ambayo imekuwepo tangia kipindi cha ukoloni. Ujenzi wa barabara hii yenye takribani kilomita 54 italeta manufaa mengi ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwezesha usafirishaji wa mazao ya wananchi katika maeneo haya ambao wengi ni wakulima wa mazao kahawa pamoja na mazao mboga mboga. Pia itachochea ukuaji wa shughuli za kiutalii na kuinua kipato cha watu na taifa kwa ujumla kupitia utalii.

Nikuombe sana, kuanzia awamu zote za uongozi wa nchi hii, ahadi za ujenzi wa barabara hii zimekuwa zikitolewa pasi na kufanikisha. Wakati huu ambao tuna kauli mbiu ya 'Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania - kazi iendelee', ni wakati sasa wa kuikumbuka na kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami. Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii kutarahisisha mawasiliano ya barabara na kuunganishwa kwa pamoja wilaya za Arumeru, Siha, Hai, Longido na nchi jirani ya Kenya.

Nimeambatanisha picha kuonyesha ubovu wa barabara hii hasa kipindi hiki cha mvua ambacho haipitiki kabisa.

Wasalam!
IMG-20210408-WA0086.jpeg
 
Poleni wananchi wa huko,nilimsikia naibu waziri wiki iliyopita akiizunhumzia hiyo barabara ila aliongea KISIASA kuwa barabara zote zitajengwa ila kwa utaratibu wa moja baada ya nyingine,zamu yenu unaweza kuwa 2045.
 
Back
Top Bottom