Kero no. 1 ya Muungano ni kuzuia kutoujadili

babykailama

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
251
243
Hainiingii akilini kuzuia Watanzania kujadili kama wanataka Muungano au la kisha kama wanautaka waseme wa aina gani. Kila siku tumeona Wazanzibar wakisema tunawaonea na sasa karibu nakubaliana na hilo maana kwa nini watu wasiruhusiwe kujadili kama wanataka huu Muungano. Ni nini hicho kinachokuwa protected kiasi hicho tusichokiona sisi? Kama ni suala la kiusalama sasa wale vijana wa Zenj wameshasema kuwa wako tayari kujilipua!!! Hii ni hatari sana.

Ukiachilia mbali mihadhara kadhaa inayotoa vitisho vya kuhatarisha hali ya usalama, hata katika Malumbano ya Hoja (ITV) Wazenj wamemalizia kwa kumzomea mzee anayesifika na mwenye heshima zake ndg. Mkinga alipojaribu kuwafundisha eti maisha yao yanategemea Bara. Hata wale wadada wameitimisha kipindi hicho cha ITV huku Wazanzibar (na wa- Bara wengine wenye upeo wa kuona tunakoelekea) wakiongea tu kwa nguvu as a way of protesting kinachopigiwa debe (the Union at all costs)!

Wa-Bara, lets wake up! yaani sisi hakika ndo tuna kero kibao.

1. Rais wangu anachaguliwa pia na Wazenj, mimi sithubutu kuwachagulia wao
2. Bajeti na mipango yangu (isiyo kwenye Muungano) Wazenj wanaijadili Bungeni lakini mimi sina mwakilishi wangu kujadili mambo yao yasiyo ya muungano katika Baraza lao.
3. Wao wana katiba yao, bendera yao n.k mimi sina hizo alama za asili za Mtanganyika ; nimebaki mkiwa mtoto yatima asiye na alama yeyote!
4. Kutukanwa kila kukicha kuwa sisi wa- Bara tunawadhulumu wazenj, kwamba tumewameza na tumewakilia!

Watanganyika tuamke na tutajadili na kuilazimisha Tume kuwa, kabla ya hiyo Katiba ya Muungano kwanza tupigishwe kura wote kuamua kama tunataka huo Muungano na uwe wa namna gani pili nataka nchi yangu Tanganyika irejeshwe maana niliyeungana naye hataki tulivyoungana na ananitukana kila kukicha.

Natamka kuwa endapo wale vijana wanatishia (angalia video huko Utube na nyingine zimeletwa hapa ) kujilipua watafanya hivyo basi tutawashitaki Viongozi wetu KWA KUSHINDWA KUCHUKUWA HATUA MADHUBUTI AMBAZO NI KUWARUHUSU WANANCHI WAJADILI JUU YA MUUNGANO WAO KWA AMANI. Mbona Viongozi wetu wanashabikia Sudan ya kusini ambayo hata haikuwai kuwa nchi huru kama Zanzibar? Waachwe wajitawale wenyewe ndipo baadaye watakumbuka umuhimu wetu na hapo ndio tutaheshimiana siku za usoni. :A S-cry:
 
Back
Top Bottom