msani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 1,801
- 1,191
Tatizo la Usafiri DSM bado ni kero kubwa sana.
Serikali ilikuja na mpango wa kutatua tatizo la usafiri dsm kwa kuanzia UDART kwa barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi kivukoni, kariakoo, na Morroco, na hivi majuzi wakaanza kufaulisha kuelekea Muhimbili, na pia kutoka Mbezi hadi kimara mwisho.
Matarajio ya wengi ilikuwa ni kupunguza tatizo lakini kwa tathmini ya haraka kwa yaliyonikuta kimara ingawa sio mkazi wa huko ila jumatatu hii nilianzia safari huko. Kwakweli naomba niseme kuna tatizo kubwa sana limeongezeka.
-Watu wanakaa muda mrefu sana kituoni. Yaani mimi nilikaa lisaa lizima nasubiri gari
-Idadi ya magari ni machache mno
-Watu ni wengi sana sana wanapigania magari na wala sio kugombea tena.
-Upatikanaji wa tiketi ni shida kubwa.
Najua kuna watu watakuwa wanatoka mbezi wanahitaji kufika ubungo au sehemu yoyote isiyozidi ubungo basi nashauri UDART waruhusu gari zao zisiishie Kimara mwisho bali zifike ubungo, yaani kutoka mbezi zishushe hadi ubungo kwani watakuwa wamepunguza tatizo.
Idadi ya magari iongezwe.
Naamini kuna kero nyingi mno mno na sisi watumiaji tunaweza kuwasaidia ili kuboresha hali ya usafiri kupunguza kero kama lilivyokuwa lengo la serikali ya JK.
Tuwashauri tu hapa
Nawasilisha