Kero na adha kubwa leo mpaka wa Tanzania na Rwanda

kwisha kazi

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
690
321
Hivi karibuni manager wa TRA hapo mpakani alipangiwa mwingine na tayari yupo eneo la kazi.Na km ilivyo ada,kila mkuu ktk eneo husika huwa na taratibu na mambo mapya hii ni bila kuvunjwa kwa kanuni na miiko ya kazi.
Tokea Juzi afisa huyo mteule alielekeza kwa aaminivyo yeye utaratibu mpya wa namna ya magari yanavyotakiwa kukaguliwa na km nilivyosema hapo awali, utaratibu huo mpya unafanywa bila kuathili miiko ya kazi.
Ajabu maafisa wakaguzi wao hawakubaliani na utaratibu huo mpya na wanadai utaratibu wa zamani aendelee jambo ambalo kuanzia mapema leo asubuhi limeathili na kuwapotezea mda mwingi madereva hasa wabebao kontena!Utaratibu huo mpya inaonesha dhahili ni pigo na hatari kwa masilahi ya mawakala wa mizigo na maafisa wa TRA wasio waaminifu na wanaoshirikiana na wenye mizigo kuvusha mizigo isiyo halisi km ilivyo ainishwa ktk nyaraka za mzigo husika.
Wito kwa mkurugenzi wa forodha na kamishina mkuu wa TRA,fuatilieni hili jambo mara moja.Maafisa wakaguzi hawa wanafanya mgomo baridi ili wamkomoe mteule wenu.Hivi hadi wakati huu majipu hayo ya shift ya asubuhi hadi mchana wameamua kupiga soga na kuwapotezea mda madereva.
Mh Rais ni haki na sawa tu kuendelea kuyatumbua tu majipu ya aina hiyo.
 
Back
Top Bottom