Kero mpya ndani ya mchakato wa katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero mpya ndani ya mchakato wa katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by jamesbond007, Aug 25, 2012.

 1. jamesbond007

  jamesbond007 Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​* New Finance Bill yapitishwa kwa mbwembwe Bungeni
  * Magari zaidi ya 800 yakwama Bandari ya Dar – Tanganyika
  * Viongozi wa Zanzibar GNU wanasema ‘hawajui, hakuna ushahidi’.
  * Imezidisha na kuzaa kero (karo) mpya ndani ya Mchakato mpya wa Katiba

  Kama mmefuatilia kwa makini, Agosti 16-2012 Bunge la jamhuri ya muungano lililokutana Dodoma limepitisha kwa ‘mbwembwe’ zote ‘The Finance Bill 2012′ – iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha wa Tanganyika, Dr. William Mgimwa.

  Sasa, kwa ufupi bill hii moja kati ya vipengelea vilivyomo ni kuwa inataka uingizaji wa magari TZ iwe ni /si chini ya miaka 10 tokea kutenngezwa kwake. Kwa maana hiyo yote yatayoingizwa nchini zaidi ya miaka kumi yatattozwa ushuru mkubwa plus ushuru wa vyuma chakavu.

  Bill hii inazungumzia ‘uingizaji wa magari kutoka nje ya nchi’ — import.

  Bill hii, kasoro yake haikutoa hata muda wa kuvuta pumzi kwa importers kinyume na taratibu za utungaji wa sheria zote duniani au hata hapa TZ.

  Yaani kama meli haijafunga gati, basi ikifika kama zimo gari za namna hiyo pia utalipa ushuru huo mpya.

  Lakini mbaya zaidi ni kuwa magari kutoka zanzibar pia yameathirika kwa maana kuwa yanatoka ‘nje’ ya nchi – Je, zanzibar ni nchi tofauti au ni nchi moja kinadharia pale wanapotaka kutumaliza? ndio inakuwa Zanzibar na Tanganyika (tanzania ni moja)?

  Hivi sasa Dar port wamezuia magari yapatayo 800 eti yameingizwa kinyume na taratibu na lazima yalipiwe huo ushuru wa vyuma chakavu, mengine yameingizwa hata kabla ya tarehe hiyo. jamani kweli haki hiyo?

  Magari mengine waliyazuia hata kabla sheria hii haijapita kwa kujua kuwa watawakomoa Wazanzibari.

  By definition, magari haya yatakuwa yameshaingia nchini (kama tunaamini zanzibar-tanganyika-tanzania ni nchi moja), unless tuamini kuwa zanzibar ni ‘foreign country’ kwa hili.

  Wenzetu hawa wanaamua mapema, kutumaliza within the process katiba mpya kero za muungano zinazidi . na karo za /KARO za MUUNGANO zinazidi kunuka; hakuna msafisahji.

  Wakati haya yanajiri, viongozi wetu wanaoshughulika na wizara za fedha na biashara wanasema ‘hawajui, hawana taarifa’ na mmoja alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa ‘anataka ushahidi’. Wafanya biashara wamempelekea ushahidi, so what? and what next? amebaki kupwesa tu kama pweza!

  Hawa ndio viongozi wetu wa GNU, wanajua kupayuka tu pale BLW na kuchukua allowance ya 600,000 per day plus other benefits – wanahalalisha matumizi yao binafsi, but utapokuja suala la nchi – forget about it – si Othman Massoud, si Mazrui au Yussuf Mzee; au Jussa-Hamza – wote hawa ni fitna tu: hawana ukweli.

  Basi hawawezi hata ku-protest kidogo hivi?

  Nakumbuka wakati wa Uongozi wa Dr.Salmin Tanganyika walizuia makontena ya Zanzibar 40 wakati ule. Waziri wa Fedha alikuwa hayati Prof.Kighoma Malima.

  Na zanzibar alichachamaa na Malima aliiitwa Zanzibar, naam…makontena yalitoka tena BUREEEE (Nassor Mazrui anakumbuka maana alikuwa President wa Chamber of Commerce); leo anatamka kuwa ‘eti hajui wala hana habari’. Ulwa mbaya baba!

  Sasa jamaa zetu wamelewa madaraka – in the GNU.

  Mwisho, namuomba adm/au shak kiongozi – kama ataipata hotuba hii ya bajeti akurushieni mzalendo, muweze kuisoma na kufaidika nayo zaidi – gazeti la zanzibar waliichapisha hii/tolea lake ya Agosti 19-2012.

  Mkumbuke kuwa Naibu waziri wa fedha anaitwa Saada Mkuya (mzanzibari), nilidhani atatetea maslahi ya zanzibar ndani ya muungano; kumbe ni figure head tu — hawashi, hazimi. yupo yupo yupo tu! anakula zake.

  * KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
  * ZIDUMU FIKRA ZA BALOZI SEIF ALI IDDI NA FIKRA ZAKE ZA SERIKALI MBILI KUELEKEA MOJA.
  * LIDUMU JIMBO LA KITOPE
   
Loading...