Kero kumi za Usafiri wa Mwendokas DSM

MR.NOMA

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
338
502
1.Ukiingia kituoni unaweza kusubiri gari hata zaidi ya nusu saa usifanikiwe kusafiri
2.Haja ndogo/ kubwa ikikubana ukiwa ndani ya kituo inakupasa kutoka nje utafte sehem ujisaidie urudi ukate tena tiketi nyingine uingie
3.Kwa sasa Magari hayo yanajaa sana,kiasi kwamba imekuwa karaha.watu kulundikwa kama mizigo.
4.Vibaka wanaendelea kutuliza simu/ waleti kila uchao
5.Joto ni Kali mkiwa mmejazana na wahusika wa magari hayo hawafungui hata vile vidirisha vya juu.
6.Kuna madereva hazimo sawa kichwani wamekuwa wakifunga milango ghafla na kuwabana abiria Mara kadhaa.
7.Abiria wa kutoka Kinondoni to kimara kubwagwa pale ubungo terminal,na kuhangaika hata saa nzima kutafta usafiri wa kwenda Kimara.
8.Wanawake wengine kujitegesha ili wabambiwe makusudi,alaf azue tafrani kuwa unambambia.
9.Express ya kutoka Kimara to Kivukoni/ Gerezan kutosimama Magomeni wakati wanajua kuna junction.
10.Watu kuingia kwa fujo,huku wakisukumana.Ikitokea umedondoka huponi.
 
Mkuu umesahau kero moja kubwa sana, kutopatikana zile kadi zao za abiria toka zilipoisha awamu ya kwanza! Na wakiulizwa wanajibu kisiasa kuwa eti kadi zile zinatengenezwa Ubelgiji hivyo tuvute subira zitakuja. Huwa najiuliza ni technology gani inayotumika kutengeneza zile kadi ambayo hapa kwetu haipo mpaka zitengenezwe huko Europe! OK sawa tufanye kuwa hatuna hiyo technology, ndio hiyo process ichukue zaidi ya mwaka mmoja? Yaani wanawasumbua watu kukaa foleni kila siku wakati kadi zingekuwepo ni suala la ku-scan na kusubiri usafiri.
 
Aisee naona leo ni siku ya kutoa dukuduku juu ya mwendokasi
 
Vituo vina space kubwa ila haitumiki. Kwa nini wasiweke coffee shops na washrooms? Kisa halijafanyika ulaya basi nao hawafikirii kulifanya.
 
1.Ukiingia kituoni unaweza kusubiri gari hata zaidi ya nusu saa usifanikiwe kusafiri
2.Haja ndogo/ kubwa ikikubana ukiwa ndani ya kituo inakupasa kutoka nje utafte sehem ujisaidie urudi ukate tena tiketi nyingine uingie
3.Kwa sasa Magari hayo yanajaa sana,kiasi kwamba imekuwa karaha.watu kulundikwa kama mizigo.
4.Vibaka wanaendelea kutuliza simu/ waleti kila uchao
5.Joto ni Kali mkiwa mmejazana na wahusika wa magari hayo hawafungui hata vile vidirisha vya juu.
6.Kuna madereva hazimo sawa kichwani wamekuwa wakifunga milango ghafla na kuwabana abiria Mara kadhaa.
7.Abiria wa kutoka Kinondoni to kimara kubwagwa pale ubungo terminal,na kuhangaika hata saa nzima kutafta usafiri wa kwenda Kimara.
8.Wanawake wengine kujitegesha ili wabambiwe makusudi,alaf azue tafrani kuwa unambambia.
9.Express ya kutoka Kimara to Kivukoni/ Gerezan kutosimama Magomeni wakati wanajua kuna junction.
10.Watu kuingia kwa fujo,huku wakisukumana.Ikitokea umedondoka huponi.

Ongezea

1. Abiria wanasubiri usafri uje, wao wamepak wanawaangalia tu. Au vituo vya katikati mabasi yanapita kwa speed kubwa huku yakiwa tupu ili hali, vituoni kuna mlundikano!

2.Speed kubwa ya hao madereva wnapo karibia kituo na kusimama ghafla huku akijua atasimama, hupelekea hata zile kamba za kujishikia kukatika njema ya msongamano kusukumana!
 
Back
Top Bottom