A
Anonymous
Guest
Habar za majukumu poleni na kazi ngumu ya kujenga taifa na kufichua uovu.
Mimi ni mfanya kazi na nimepita sehemu mbali mbali.
Lakini nimefanya kazi mkoa wa mwanza ,wilaya ya ukelewe kijiji cha ukala chenye vitongoji 8 kama vile Bwisya, Nyang'ombe, Chilled, Chibasi, Kome, Bukiko na Nyamanga.
Huku kuna kero kubwa 3:
Umeme:
Kuna kampuni inayotoa umeme inayoitwa Jumeme. Hakika wananchi wanateseka sana na umeme, ambapo umeme huu ni wa sola, na kampuni inayohusika ni Jumeme.
Ratiba ya umeme ni ngumu sana umeme wanakata saa 4 usiku au saa 3 na unarudi kesho yake saa 4 asubuh na ikifika saa 10 jioni wanakata tena na unarudi saa moja jioni. Kwa sababu, ukifatilia wanakwambia battery zetu zina shida hivyo tunazima ili tusitumie sana lakini wakati huo huo ikisemekana kuna kiongozi yoyote wa Serikali anakuja umeme haukatiki hata kidogo hata kama ni siku 3, umeme haukatiki.
Na kingine wasimamizi wa kampuni ya Jumeme hasa Bwisya ni shabiki wa Simba, ikitokea Simba anacheza siku husika umeme haukatiki hata kidogo na mpira ukiisha wanakata. Na kama yanga anacheza siku hiyo umeme wanakata. Hii inamaanisha kuwa na watu wanaofanya vitu kwa makusudi.
Kingine ni kuwa, ukinunua umeme wa elf 5 unapata unit 2 tu umeme una gharama kubwa sana na makubaliano ya umeme ilikua ni masaa 24 umeme haitakiwi ukatike na ikitokea ni kipindi cha mvua basi watatumia generator lakini kimsingi hakuna uhalisia wa huduma na hakuna kiongozi yoyote anaewajibika sio mkuu wa wilaya wala TANESCO.
Mambo mengine ni Maji na Mitandao ya simu - vyote havifanyi kazi kabisa.