KERO: Kitu hiki kinanikera sana kwenye kumbi zetu hizi za kuangalia mpira

Hahaaa tatizo ni pale unapomuuliza nani kafungwa hata hakujibu utashangaa kapanda juu ya benchi.
 
Kwanza kabisa, namshukuru Mungu kwa ajili ya neema zake & jumapili iliyo njema katika kuadhimisha siku yetu wafanyakazi.

Pia niseme tu kuwa, mimi ni mpenzi wa michezo hasa mpira wa miguu. Na kutokana na ili na lile napenda kwenda kutazama mpira hasa huu wa Ulaya, mainly EPL/BPL. Na huwa naenda sehemu za mikusanyiko, tunaita ukumbini.

Sasa, kuna hii tabia huwa INANIKERA sana na kupelekea kuondoa hamu ya kutazama mechi.

Kuna redio hutangaza matangazo ya mpira sambamba na TV zinazorusha live. Sasa, redio huwahi kutangaza goli kabla hujaona kwenye TV (Wataalamu wa fani wanajua zaidi).

Kuna watu wanaingia na viredio vyao au wanatumia simu kwa kutumia earphones. Sasa, goli likifungwa wanawahi kushangilia kabla hatujaona kwenye TV. Au mtu akikosa, utasikia anainuka anapiga kelele wakati kwenye TV muda huo mpira ndo uko huku nyuma.

Yaani wenyewe ndo wanakuwa INDICATOR wetu; Ina maana tukiona kimya, tunajua hamna kitu huku. Ukiwaambia kuzima redio, wanakuwa wabishi kweli.

Na wengine walio BET wako online muda wote, ambapo score board inabadilika kwa haraka kabla TV haijaonyesha ... Utasikia wanashangilia.

Hii inapelekea kuondoa radha kamili na maana nzima ya kwenda KUTAZAMA mpira. Zimeni redio, au mbaki home msikilize. Mnaboa sana aisee.

Sasa, leo Man U inakipiga na mabingwa watarajiwa Leicester City & muda huu najiandaa kusogea huko.

Niwaombe, tena kwa dhati msije na REDIO zenu ili tuenjoy game.

Nawatakia muda mwema.
Ni kweli. Hiyo tabia inakera. Ni dalili ya ushamba tu na si kingine. Kwa kifupi wanaofanya hivyo ni washamba!
 
Back
Top Bottom