Kero: HESLB kuweni makini katika loan transfers

Kero: HESLB kuweni makini katika loan transfers

avi.JNR

Senior Member
Joined
Nov 17, 2015
Posts
139
Reaction score
87
Hivi kuna haja gani ya kuwapa Mikopo wanafunzi wa VYUO VIKUU? SI kujikimu au? Sasa mwanafunzi wa chuo kikuu kafanya
Transfer au Declined na chuo husika ukiwa tayari kashapata mkopo kwenye chuo alichochaguliwa mwanzo? Hapo ugumu uko wapi kutransfer loan yake?

Unamwambia mwanafunzi nasubiri siku 60. JE, UNAJUA kuwa hiyo ni miezi miwili?

JE ushajiuliza kuwa SEMISTER INA MIEZI MINNE, sasa hiyo miezi miwili ale nini? Akae wapi Ikiwa walio wengi wanatoka MIKOANI?

Swali langu kwa HELSB ni data gani zinahamishwa muda wa miezi miwili ili wanafunzi wapate hizo pesa? Au ndo mnazungushia biashara zenu baada ya Miezi miwili ikiisha mnawapa?

Swali lingine hao wanafunzi mnataka wasome vipi bila hizo loan walizoomba na mkawapatia? Na Ikiwa wanafunzi wanaofanya Transfer hawazidi 900 TU?

KUWENI NA HURUMA KIDOGO .SISI WENGNE TUNASOMA KWA FULL ACCOMODATION LAKINI WENZETU WANAPATA SHIDA
 
kwakweli wanakera sana. hapa Tanzania kila kitu ubabaishaji tu. tumechoka. nawapa pole wahanga wa tatzo hili. nilipokuwa Chuo nilimpa sapoti rafiki yangu kwa ttzo kama hili. tulijibana sana wakaja kumpa baada ya miezi mitatu. loan officer wa pale Chuo nae alikuwa hafuatilii kabisa. loan board waliangalie hili jipu kwamaana limeoza mpaka linanuka.
 
kwakweli wanakera sana. hapa Tanzania kila kitu ubabaishaji tu. tumechoka. nawapa pole wahanga wa tatzo hili. nilipokuwa Chuo nilimpa sapoti rafiki yangu kwa ttzo kama hili. tulijibana sana wakaja kumpa baada ya miezi mitatu. loan officer wa pale Chuo nae kama zezeta turn alikuwa hafuatilii kabisa. loan board waliangalie hili jipu kwamaana limeoza mpaka linanuka.
Kuna dogo mmoja pia nipo naye hapa ndo kwanza wameingia .Ali transfer ..hana hata pesa ya kula ..kwani kinachowafanya wachelewe nini Ikiwa pesa walishatengewa ...kwakuwa walitransfer .basi wanatakiwa kupata data full kwa chuo walikosajiliwa na kuamisha pesa .basi .hakuna kingne sasa .wao eti siku 60 . za nn** watu wanashindwa kusoma huku .na sisi tunawasaidia tunachoka wawape hela zao zipo
 
ndugu ebu nisaidieni hapo iyo miezi miwili wanaesabu kwanzia lini pindi umefanya transfer au watakapo pata taarifa zako toka kwa loan officer chuo husika ulichoomba transfer maana nashidwa elewa hapo inakuwaje
 
ndugu ebu nisaidieni hapo iyo miezi miwili wanaesabu kwanzia lini pindi umefanya transfer au watakapo pata taarifa zako toka kwa loan officer chuo husika ulichoomba transfer maana nashidwa elewa hapo inakuwaje

Wanaesabu pale wanapopata taarifa za APPLICANT aliye transfer kwa mujibu wa maelezo yao.
 
Wanaesabu pale wanapopata taarifa za APPLICANT aliye transfer kwa mujibu wa maelezo yao.

nimekuelewa ndugu ila sasa ma loan officer wakichelewa kupeleka taarifa zako uko bodi ndio mtu inakula kwako unaweza maliza mwaka wa kwanza bila mkopo kabisa
 
Sasa nini maana ya kujiita tuko ulimwengu wa digitali kama jambo dogo kama hilo tu wanasema siku sitini magufuli si ayafukuze tu maana wameshindwa kwenda na wakati watu tunakuwa maparisite huku chuoni mpaka aibu kwani hizo hela zilipelekwa sayari ipi mpaka iwe siku stini
 
Mr.president tunaomba utembelee heslb mapema ...hawa watu hawako makini na kazi
kuna watu wa mwaka wa pili, walikuwa wanalipiwa ada mwaka jana lkn cha ajabu mwaka huu wamewekewa 0.
wengine majina yao hayajatoka mpk leo wakati mwaka jana wamepata hela yao vizuri tu..
 
bora na hao wa transfer mimi hapa nime sighn boom trh 15 mpaka leo sijapata pesa wala sijui hatima yangu

Nipo udom first year.
 
daah! nilijua mm tu wakuu, yan inakera, wakati mwingne niliona elimu haina maana, nahaso knyama
 
Hivi hawa bodi ya mikopo mbona ni complicata sana wanatulaza njaaa pasipo hatia mungu wangu na madeni makubwa nashindia chai nashindwa kusoma vzr hakika nateseka namuomba my president JPM awaangalie bodi ya mikopo kuuhamisha mkopo wakati mmepata taarifa kutoka chuoni kwake kwamba yupo sio siku 60 kwa watu makini ni siku 1 tu mnategemea tuishije ?
 
Yaaaani inaniuma sana bodi ya mikopo leteni mikopo yetu vyuoni kama taaarifa mmeshapewa mnangoja nini Mimi mpaka sasa sijala najiombeleza hela kwa Msela kama yatima jamaaa nae anacheka tu hapa wakati mkopo wangu upo
 
Yaaaani inaniuma sana bodi ya mikopo leteni mikopo yetu vyuoni kama taaarifa mmeshapewa mnangoja nini Mimi mpaka sasa sijala najiombeleza hela kwa Msela kama yatima jamaaa nae anacheka tu hapa wakati mkopo wangu upo

Huyu msela lakini si alikupa au..na mrudishie ukopata boom..
 
Twendeni kwenye vyombo vya habari vitusaidie kufikisha kilio chetu kwa jamii nzima.Tukilalamika tu humu haisaidii kitu.Mimi binafsi nimeshateseka sana na bado naendelea kuteseka tu.
 
Bodi ya mikopo nimechoka kusubiri mkopo wangu muulete mbona kimya mpaka sasa uleteni niusani Mnanitesa sana
 
Back
Top Bottom