Kenyatta akubali kukutana na Nasa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Nairobi, Kenya. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema yuko tayari kukutana na wapinzani kutoka muungano wa Nasa lakini akasema atakuwa tayari kufanya hivyo iwapo mazungumzo yao yatakuwa na lengo la kuikwamua Kenya na wala siyo kujadili siasa.
kinya.jpg

"Niko tayari kwa mazungumzo na yeyote," alisema Rais Kenyatta wakati akizungumza katika kongamano la magavana ambapo aliahidi kushirikiana nao kuimarisha Kenya.

Kongamano hilo liliandaliwa ili kutoa mafunzo kwa magavana wapya, ikiwa ni pamoja na kuchagua mwenyekiti mpya wa baraza la magavana.

Gavana wa Turkana, Josphat Nanok ndiye mwenyekiti wa baraza hilo kwa sasa na atatetea kiti chake kinachomezewa mate pia na Gavana wa Kwale, Salim Mvurya. Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru anamezea mate kuwa naibu mwenyekiti wa baraza hilo.

Katika hotuba yake Rais Kenyatta alisisitiza kuwa mazungumzo anayotaka na Nasa ni ya kuendeleza taifa na siyo kujadili kuhusu siasa. Awali, alisema siasa zitajadiliwa mwaka 2022 ambapo Naibu Rais William Ruto anatarajiwa kupeperusha bendera ya Jubilee (JP) kuwania kiti cha urais.

Rais Kenyatta hata hivyo, alisema sheria zilizomo kwenye katiba sharti zifuatwe katika kila hatua kufanya mazungumzo na kuendesha taifa mbele.

"Kila tunachofanya kiegemee kwa msingi wa katiba. Watakaofanya nje ya katiba na sheria za nchi watakabiliwa vilivyo," alionya kiongozi huyo.

"Serikali yangu haitaruhusu yeyote atakayecheza na kuhatarisha maisha ya Mkenya ama kuharibu mali yake. Hiyo laini ukipita, sheria ni sheria itachukua mkondo wake," alisema.

Aliahidi kufanya kazi na kila gavana licha ya mrengo wa kisiasa anaoegemea. Jumapili iliyopita kinara mwenza wa Nasa, Musalia Mudavadi alisema muungano huo unaomba kufanya mazungumzo na Serikali ya Jubilee ili kujadili uwezekano wa kuandaliwa kwa uchaguzi mwingine.

Aliyekuwa waziri mkuu, Raila Odinga hivi karibuni aliahirisha mipango yake ya kuapishwa kama wa wananchi na kusema kazi hiyo itafanyika baadaye bila kutaja tarehe.


Chanzo: Mwananchi
 
Hili mbona ameliesema siku zote, kwamba yupo radhi kujadili maendeleo na sio mifumo ya kisiasa, ila pia hawezi kukwepa maongezi ya kisiasa maana kiti chake hicho ni cha kisiasa. Asiwe kama marais ambao kwao wamekataza mikutano yoyote ya kisiasa lakini hao hao marais wanahutubia mikutano huku wakirusha madongo ya kisiasa.

Nchi hii tunafaa tuwekane sawa kwenye suala la uchaguzi, tuache haya mambo ya kila wanaoshindwa wanaanza kuigawa nchi, lazima tutafute jinsi ya kuhakikisha wanaoshindwa wanabaki wakihisi ni Wakenya ndani ya Kenya.
 
Back
Top Bottom