Kenya Yazindua Reli yake iliyojengwa na China

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,292
Nchi ya Kenya imezindua reli yake iliyojengwa na nchi ya China.

Mradi huo ni mradi mkubwa kuliko yote wa Kwanza kufanywa nchini Kenya tangia uhuru.

Source:

China-built railway biggest Kenya project since independence

Associated Press
TOM ODULA 1 hour 51 minutes ago
MOMBASA, Kenya (AP) — Kenya's president on Tuesday opened the country's largest infrastructure project since independence, a Chinese-backed railway costing nearly $3.3 billion that eventually will link a large part of East Africa to a major port on the Indian Ocean as China seeks to increase trade and influence.

The railway replaces part of the 660-mile (1,062-kilometer) line known as the "lunatic express," which was built by the British more than a century ago and linked Lake Victoria with the port city of Mombasa. Kenya Railways says the newly opened stretch will reduce passengers' travel time from the capital, Nairobi, to Mombasa from more than 10 hours to four.
 
Hongera sana jirani, nasi soon ngosha atatufikisha huko.....just a matter of time!
pamoja na mapungufu yake lakini still he's far far better kuliko hawa matapeli wanaojiita wapinzani!!
 
Mabasi yanakosa kazi
hio target yao sio abiria japokuwa watakuwemo ila hio ni kwa ajili ya mizigo kutoka bandari ya mombasa. na project hii ina connect south sudan , uganda na rwanda.
Bandari ya Mombasa imechaguliwa kuwa moja katika project ya Marine silk route kwahiohio treni wachina wamesaidia kwa sababu zao na watafaidika sana wakenya waganda na south sudan pamoja na rwanda
 
Wakaichagua na Bagamoyo ili kuhudumia Great Lakes Region pamoja na nchi za Malawi na Zambia. Hapa Watanzania, kama ilivyo ada; tumeleta siasa!!! Na kuna kila dalili Wachina wakaachana na Bagamoyo Project na kurudi Lamu ambako walikusudia hapo awali!!!
 
Ikiwa bagamoyo ilichaguliwa basi sahivi wachina washaachana nayo wala hawana mpango nayo tena.
maana wiki mbili zilizopita wachina wametangaza bandari pekee ya africa mashariki kushirikishwa katika hio marine silk route ni bandari ya mombasa tu.
kwahiyo sahivi tanzania mizigo yetu tutakuwa tunachukua kutoka bandari ya mombasa kutoka china na baadhi za nchi kutoka europe, southeast asia na pacific
 
Hongera nyingi sana kwa Kenya na President Kenyatta.

Tanzania tumeweka jiwe la msingi la SGR kwa mbwembwe kumbe hata hela za ujenzi wa hiyo reli hakuna.

Kila Rais anaekuja kutembelea Tanzania hata kama ametokea Chad anaombwa mkopo.

Wa mwisho kumuomba hapa karibuni ni Zuma.. tunasubiri atuombee hela za mkopo kwa washirika wake...!!

Very shame.
 
Hii ni ndoto ya mchana au sijuwi miseme usiku. Kwahiyo unatuaminisha shaba ya Zambia itabebwa juu mpaka badari ya Mombasa au Lamu. Badari zetu za Tanzania zinanza kubadili upepo, badala kurumika kupokea mizigo zaidi, zinatumika kusafirisha mizigo nje. Tanga waneshaanza kujikita na mafuta ya Uganda pamoja na Congo, Dar viwanda vya mkoa wa pwani, Morogoro na bidhaa za nchi zingine. Mtwara wao gesi na bidhaa zinazo tokana na gesi pamoja na chuma cha Liganga. Zanzibar bandari huru. Sasa tumepungukiwa na nini au bado mnatala turudi kwenye ukoloni mambo leo wa wachina?
 
a big blow for Tanzania...especially since the China Road project has put Kenya as the manin stop in Africa....Rwanda Burundi Uganda na South Sudan hawana budi kutumia bandari la Mombasa...finally, reli ya Tz bado ndoto...hakuna pesa za kujenga reli hii...dah! wakenya sio watu mchezo mchezo
 
Hii ni ndoto ya mchana au sijuwi miseme usiku. Kwahiyo unatuaminisha shaba ya Zambia itabebwa juu mpaka badari ya Mombasa au Lamu. Badari zetu za Tanzania zinanza kubadili upepo, badala kurumika kupokea mizigo zaidi, zinatumika kusafirisha mizigo nje. Tanga waneshaanza kujikita na mafuta ya Uganda pamoja na Congo, Dar viwanda vya mkoa wa pwani, Morogoro na bidhaa za nchi zingine. Mtwara wao gesi na bidhaa zinazo tokana na gesi pamoja na chuma cha Liganga. Zanzibar bandari huru. Sasa tumepungukiwa na nini au bado mnatala turudi kwenye ukoloni mambo leo wa wachina?
Unajua wewe ni mtu wa ajabu kama sio mtu wa hovyo hovyo?!

Hapa tunazungumzia miradi ya ujenzi na sio political hallucination! Ndoto za Zanzibar kuwa Free Port zilianzishwa na Salmin Amour zaidi ya miaka 15 iliyopita lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika!!!

Mradi wa bomba la mafuta Tanga umekuja by chance baada ya Total kushituka dakika za mwisho kutumia bandari ya Mombasa!!!

Miradi ya Tanga ambayo ipo au ilikuwa kwenye pipeline ni mradi wa deep sea port na Mwambani port... mmoja ni mradi wa TPA na mwingine ni mradi wa VIP Engineering under Mwambani Port & Railway Corridor Company!!!

Huo mradi wa bomba la mafuta utakuwa na impact ndogo sana katika ujenzi wa bandari... zaidi tu ya kupanua miundombinu ya hapa na pale.

Narudia, msome niliyem-quote na soma nilichokiandika vinginevyo usingekuja na hoja za hovyo hovyo kuhoji "shaba ya Zambia itabebwa juu?" Nani amekuambia habari ya shaba ya Zambia hapa?! Btw, kwanihivi sasa inabebwa juu?!!

Hapa umeambiwa miradi ya China barani Afrika! Kwa wanaofuatilia masuala ya marine transportation wanafahamu what's going on.

China ni kama wameigawa Afrika into blocks ili kurahisisha biashara zao... hakuna aliyetaja habari ya shaba ya Zambia hapa wala magogo ya DRC!!!

Horn of Africa, wanapanua bandari ya Djibouti kisha wakajenga reli kutoka Ethiopia inayolenga kuunganisha na bandari ya Djibouti.

East Africa, Kenya walikuwa wanapigia upatu Wachina wajenge bandari mpya ya Lamu lakini wakachomoa na kuchagua Bagamoyo. Hii ingekuwa au itakuwa ndo largest port in Africa on completion.

Ili kuiunganisha na landlocked countries walikusudia kujenga reli itakayounganisha Bagamoyo na Reli ya Kati. Na kwavile lengo lao ni ku-facilitate biashara zao, walikusudia kujenga industrial zone mradi ambao ungefanywa na Oman.

Pamoja na hiyo miradi, kuna mingine kadhaa kamavile Takoradi, Ghana; Walvis Bay in Namibia, Sao Tome & Principe na miradi mingine mbalimbali!!!
 
Hahahahahaha..
Mkuu umenichekesha sana.
Zuma hajaleta bado Mkuu.
Jamaa yetu na Bashite waliweka jiwe la msingi kwa mbwembwe kumbe hamna hela.
Halafu mkuu analazimisha waandike kwenye media mradi umeanza wakati sio kweli..COWI ambao ndio ma consultant wamemkatalia wamemwambia we are not doing politics...kwa kifupi mradi hakuna kunachofanyika hela hakuna
 
Hongera nyingi sana kwa Kenya na President Kenyatta.

Tanzania tumeweka jiwe la msingi la SGR kwa mbwembwe kumbe hata hela za ujenzi wa hiyo reli hakuna.

Kila Rais anaekuja kutembelea Tanzania hata kama ametokea Chad anaombwa mkopo.

Wa mwisho kumuomba hapa karibuni ni Zuma.. tunasubiri atuombee hela za mkopo kwa washirika wake...!!

Very shame.
Kuomba omba ndiyo hulka yetu..Kikwete alizurura duniani kuomba net za mbu
 
Ikiwa bagamoyo ilichaguliwa basi sahivi wachina washaachana nayo wala hawana mpango nayo tena.
maana wiki mbili zilizopita wachina wametangaza bandari pekee ya africa mashariki kushirikishwa katika hio marine silk route ni bandari ya mombasa tu.
kwahiyo sahivi tanzania mizigo yetu tutakuwa tunachukua kutoka bandari ya mombasa kutoka china na baadhi za nchi kutoka europe, southeast asia na pacific
Anyway, siwezi kushangaa and I expected this soon baada ya mradi wa reli kuwapa Wataruki!!

Si kwamba Wachina walikuwa na haki ya kupewa huo mradi wa reli lakini Wachina mambo yao ni fasta fasta! Walitaka mradi wa reli na Bandari ya Bagamoyo iende pamoja na imalizike kwa wakati! Exim Bank ya China walishakuwa tayari ku-finance hizo projects.

Lakini baada ya kupeleka mradi kwa Waturuki, ndo kwanza tumeanza na Phase I hadi Morogoro huku tukijifanya tutajenga kwa pesa zetu!! Hapo Mchina lazima aone unataka kumchelewesha.

So, best wishes kwa wapwa zetu Kenya! Na uzuri wa Kenya kwa sasa; every possible president ni bepari la kuzaliwa! Akirudi Kenyatta ni bepari la kuzaliwa na akichaguliwa Odinga nae ni bepari la kuzaliwa!!

None of these two anaweza kuacha big projects zi-skip kirahisi rahisi tu!!!

Wakati Total wanabadili mawazo kutoka Mombasa to Tanga, niliwaambia watu hapa Kenyatta will never stop hadi anaona bomba la kwanza linatandazwa ardhini!!!

That's how a president needs to be!!!
 
Wakaichagua na Bagamoyo ili kuhudumia Great Lakes Region pamoja na nchi za Malawi na Zambia. Hapa Watanzania, kama ilivyo ada; tumeleta siasa!!! Na kuna kila dalili Wachina wakaachana na Bagamoyo Project na kurudi Lamu ambako walikusudia hapo awali!!!

Unajua wewe ni mtu wa ajabu kama sio mtu wa hovyo hovyo?!

Hapa tunazungumzia miradi ya ujenzi na sio political hallucination! Ndoto za Zanzibar kuwa Free Port zilianzishwa na Salmin Amour zaidi ya miaka 15 iliyopita lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika!!!

Mradi wa bomba la mafuta Tanga umekuja by chance baada ya Total kushituka dakika za mwisho kutumia bandari ya Mombasa!!!

Miradi ya Tanga ambayo ipo au ilikuwa kwenye pipeline ni mradi wa deep sea port na Mwambani port... mmoja ni mradi wa TPA na mwingine ni mradi wa VIP Engineering under Mwambani Port & Railway Corridor Company!!!

Huo mradi wa bomba la mafuta utakuwa na impact ndogo sana katika ujenzi wa bandari... zaidi tu ya kupanua miundombinu ya hapa na pale.

Narudia, msome niliyem-quote na soma nilichokiandika vinginevyo usingekuja na hoja za hovyo hovyo kuhoji "shaba ya Zambia itabebwa juu?" Nani amekuambia habari ya shaba ya Zambia hapa?! Btw, kwanihivi sasa inabebwa juu?!!

Hapa umeambiwa miradi ya China barani Afrika! Kwa wanaofuatilia masuala ya marine transportation wanafahamu what's going on.

China ni kama wameigawa Afrika into blocks ili kurahisisha biashara zao... hakuna aliyetaja habari ya shaba ya Zambia hapa wala magogo ya DRC!!!

Horn of Africa, wanapanua bandari ya Djibouti kisha wakajenga reli kutoka Ethiopia inayolenga kuunganisha na bandari ya Djibouti.

East Africa, Kenya walikuwa wanapigia upatu Wachina wajenge bandari mpya ya Lamu lakini wakachomoa na kuchagua Bagamoyo. Hii ingekuwa au itakuwa ndo largest port in Africa on completion.

Ili kuiunganisha na landlocked countries walikusudia kujenga reli itakayounganisha Bagamoyo na Reli ya Kati. Na kwavile lengo lao ni ku-facilitate biashara zao, walikusudia kujenga industrial zone mradi ambao ungefanywa na Oman.

Pamoja na hiyo miradi, kuna mingine kadhaa kamavile Takoradi, Ghana; Walvis Bay in Namibia, Sao Tome & Principe na miradi mingine mbalimbali!!!
Muda mwingine jaribu kufikiri nje ya siasa, nilichoandika mimi kinahusiana nini na maswala ya siasa? Umegusia Zambia na Malawi walitakia watumie bandari ya Bagamoyo, lakini wachina wamekimbilia Kenya kwasababu sisi tumeleta siasa. First of all, mizigo ya Zambia na Malawi isinge pita Bagamoyo na wala haitakuja kupita Bagamoyo. Bandari ya Bagamoyo ilikuwa na maudhui yake tofauti na unavyo fikiria wewe.

Swala la Zanzibar kuwa bandari huru, ni swala lililo jichanganya na mambo ya muungano, kwamba kama Zanzibar ikiwa bandari huru, itachagia vipi kuzorotesha mapato ya bara. Malumbano yameenda nyuma mbele mpaka Kikwete na Sheni wakakubaliana jinsi ya kutatua tatizo zima pamoja na swala la mafuta ya Zanzibar.

Nashangaa unasema eti bandari ya Tanga haitaingiza kipato kikubwa kutokokana na mafuta ya Uganda. If that's the case kwanini wakenya wameumia sana kuukosa mradi huo? Mafuta, sisal, perishable goods, industrial goods yote hiyo unaona hakuna kipato. Mbona hujaongelea bandari ya mtwara mbayo itakuwa na reli yake mpaka ziwa Nyasa na kuudumia mizigo ya Malawi mpaka Zimbabwe.

Kinacho kuumiza hapa ni sisi kutokuchangamkia fursa za wachina. Umeshindwa kuchambuwa kwanini tumekuwa tunavuta mguu na swala la uwekezaji wa wachina. Imani yako ni kuwa wachina ni watu wakufanya vitu haraka haraka, lakini haujiulizi hiyo haraka inakuja kwa gharama gani?. Mchina anakupa mradi haraka haraka lakini gharama yake ni Mara tatu kuliko gharama halisi na hakuna uhakika kama huo mkopo utaweza kuilipa. Tunamiradi mingi na wachina lakini sio kila mradi lazima tuseme "ndio mzee"

Soma kwa makini mrejesho huu hapa chini upate mawili matatu.
Kenyans carry the burden of China's high cost loans
 
Muda mwingine jaribu kufikiri nje ya siasa, nilichoandika mimi kinahusiana nini na maswala ya siasa? Umegusia Zambia na Malawi walitakia watumie bandari ya Bagamoyo, lakini wachina wamekimbilia Kenya kwasababu sisi tumeleta siasa. First of all, mizigo ya Zambia na Malawi isinge pita Bagamoyo na wala haitakuja kupita Bagamoyo. Bandari ya Bagamoyo ilikuwa na maudhui yake tofauti na unavyo fikiria wewe.

Swala la Zanzibar kuwa bandari huru, ni swala lililo jichanganya na mambo ya muungano, kwamba kama Zanzibar ikiwa bandari huru, itachagia vipi kuzorotesha mapato ya bara. Malumbano yameenda nyuma mbele mpaka Kikwete na Sheni wakakubaliana jinsi ya kutatua tatizo zima pamoja na swala la mafuta ya Zanzibar.

Nashangaa unasema eti bandari ya Tanga haitaingiza kipato kikubwa kutokokana na mafuta ya Uganda. If that's the case kwanini wakenya wameumia sana kuukosa mradi huo? Mafuta, sisal, perishable goods, industrial goods yote hiyo unaona hakuna kipato. Mbona hujaongelea bandari ya
mbayo itakuwa na reli yake mpaka ziwa Nyasa na kuudumia mizigo ya Malawi mpaka Zimbabwe.

Kinacho kuumiza hapa ni sisi kutokuchangamkia fursa za wachina. Umeshindwa kuchambuwa kwanini tumekuwa tunavuta mguu na swala la uwekezaji wa wachina. Imani yako ni kuwa wachina ni watu wakufanya vitu haraka haraka, lakini haujiulizi hiyo haraka inakuja kwa gharama gani?. Mchina anakupa mradi haraka haraka lakini gharama yake ni Mara tatu kuliko gharama halisi na hakuna uhakika kama huo mkopo utaweza kuilipa. Tunamiradi mingi na wachina lakini sio kila mradi lazima tuseme "ndio mzee"

Soma kwa makini mrejesho huu hapa chini upate mawili matatu.
Kenyans carry the burden of China's high cost loans
We jamaa una kichwa kizito kishenzi kuelewa!!! Hivi umeambiwa mizigo ya Zambia na Malawi au umeambiwa Wachina wana projects za bandari sehemu kadhaa Afrika kwa ajili ya ku-facilitate biashara zao?!

Hebu rudia kusoma hapa:
Hapa umeambiwa miradi ya China barani Afrika! Kwa wanaofuatilia masuala ya marine transportation wanafahamu what's going on.

China ni kama wameigawa Afrika into blocks ili kurahisisha biashara zao... hakuna aliyetaja habari ya shaba ya Zambia hapa wala magogo ya DRC!!!
Halafu pamoja na kueleweshwa; bado unarudia tena jambo lile lile... mara oh, Malawi na Zambia hawawezi kupitishia mizigo Bagamoyo!!

Halafu ona hilo la Tanga!! Umeambiwa bandari ya Tanga haiwezi kuchangia mapato au umeambiwa suala la bomba la mafuta kupita Tanga lilikuja by chance baada ya Total kushituka dakika za mwisho kutumia Mombasa? Again, soma tena hapa kwa vituo:
Mradi wa bomba la mafuta Tanga umekuja by chance baada ya Total kushituka dakika za mwisho kutumia bandari ya Mombasa!!!

Miradi ya Tanga ambayo ipo au ilikuwa kwenye pipeline ni mradi wa deep sea port na Mwambani port... mmoja ni mradi wa TPA na mwingine ni mradi wa VIP Engineering under Mwambani Port & Railway Corridor Company!!!

Huo mradi wa bomba la mafuta utakuwa na impact ndogo sana katika ujenzi wa bandari... zaidi tu ya kupanua miundombinu ya hapa na pale.
Wapi nimezungumzia suala la bandari ya Tanga kuingiza kipato kidogo au kikubwa?

Hilo suala la Bandari Huru ya Zanzibar na Muungano wapi na wapi?! Umeambiwa bandari ni suala la muungano?!

Angalia kiroja chako kingine! Eti mbona sijazungumzia suala la bandari ya Mtwara! Ulitaka nizungumzie kitu ambacho hakikuwa sehemu ya mjadala??!! Kama ni mara yako ya kwanza kuingia kwenye mijadala ya bandari; kwangu mimi nishafanya hiyo mijadala mara kadhaa na ndio maana wala sikuona sababu ya kufungua hyo link uliyoweka kwa sababu hakuna cha maana utakachosema ambacho watu hatujakijadili hapa!!

Na hata hilo suala la gharama tushawahi kujadili hapa takribani miaka 3 iliyopita!! Mjadala ulihusu mikopo ya muda mrefu yenye riba ndogo lakini total ya unacholipa kinakuwa kikubwa maradufu!!!

Investment projects ni topic of my interest!! Nishajadili sana humu jamvini masuala ya bandari, reli, madini na gas na kwa kawaida, huwa siongei kabla ya kufanya utafiti!!!

Hata suala la bandari ya Mtwara nishawahi kulijadili hapa mara kibao tu siku za nyuma! Post yangu ya karibuni kabisa kuhusu bandari ya Mtwara ni ile ya February 19! Hii hapa:
Kuhusu Mtwara... uzuri wa pale ni natural habor lakini bado huwezi kuchanganya bandari ya kawaida na oil shippers terminal! Kwa gas boom iliyo kusini, biashara ikishachanganya bandari ya Mtwara itakuwa bize sana na mimeli ya kusafirisha gas na ile mimeli ni mikubwa mno... mtu akifunga nanga; wengine mnasubiri!!!

Hayo mambo ya kusubiri ndo asiyoyataka Mchina na ndio maana akaamua aanze moja! I guess hata kiusalama not advisable!

Kwahiyo, si kwamba bandari ya sasa ya Mtwara nayo inatakiwa kupanuliwa kwa ajili ya meli za mafuta lakini hata ukitaka kujenga bandari nyingine bado huwezi kujenga pale pale! Na ndio maana hata Dangote ametaka kujenga bandari yake kwa sababu inaonekana ana uzoefu wa bandari zinazohudumia meli za mafuta kwa sababu kule Nigeria zipo sana na karibu zote kama sio zote zinajengwa separately.
Hapo nilizungumzia bandari ya Mtwara kwa sababu hoja ilihusu bandari ya Mtwara!!

Hapa hoja ni bandari ya Bagamoyo we unataka nizungumzie bandari ya Mtwara... wapi na wapi! Ndo maana nikakuambia unaleta siasa!!

Unaleta siasa kwa sababu unahangaika kuonesha nini serikali inafanya na matokeo yake; unachanganya madesa! Unaambiwa biashara za Wachina, wewe unaleta habari za copper ya Zambia! Unaambiwa kutakuwa na impact ndogo kwenye ujenzi wewe unaleta habari za kuingiza kipato!!!

Soma uelewe kabla hujakurupuka ku-comment!!!

Halafu ulivyo kiroja eti inaniuma kwa sababu hatuchangamkii fursa za Wachina!! Asiyechangamkia fursa za Wachina ni nani?! Au kwa akili yako unaamini Uchina na Uturuki ni tofauti?!

Unatamba kutochangamkia fursa za Wachina halafu inakuja nchi maskini kama Ethiopia unaiomba msaada wakati na yenyewe inasaidiwa na Wachina!! Anakuja Jacob Zuma unamuomba msaada wakati hao BRICS wenyewe huwa wanapiga magoti kwa China!!
 
Nchi ya Kenya imezindua reli yake iliyojengwa na nchi ya China.

Mradi huo ni mradi mkubwa kuliko yote wa Kwanza kufanywa nchini Kenya tangia uhuru.

Source:

China-built railway biggest Kenya project since independence

China-built railway biggest Kenya project since independence

Associated Press
TOM ODULA 1 hour 51 minutes ago
MOMBASA, Kenya (AP) — Kenya's president on Tuesday opened the country's largest infrastructure project since independence, a Chinese-backed railway costing nearly $3.3 billion that eventually will link a large part of East Africa to a major port on the Indian Ocean as China seeks to increase trade and influence.

The railway replaces part of the 660-mile (1,062-kilometer) line known as the "lunatic express," which was built by the British more than a century ago and linked Lake Victoria with the port city of Mombasa. Kenya Railways says the newly opened stretch will reduce passengers' travel time from the capital, Nairobi, to Mombasa from more than 10 hours to four.
Kujengwa na China maana yake nini? Wivu ama?
 
Back
Top Bottom