Kenya yaunga mkono vikosi vya ECOWAS

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,946
3,689
Kenya imesema inaunga Mkono uamuzi wa Jumuia ya Afrika Magharibi(ECOWAS) ya kumfurusha Bw.Yahya Jammey ambaye amegeuka kuwa Muasi na kukatalia Ikulu wakati yeye sio Rais kuanzia Jana.Hayo yametamkwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Bi.Amina Mohamed.
Hata hivyo Majeshi ya ECOWAS yameshaingia Mjini Banjul baada ya Rais Mteule Bw.Barrow kuomba msaada wa kumtoa Bw.Jammey.
Kwa sasa Bw.Jammey ameomba kusamehewa Makosa yote aliyokosa kipindi akiwa Rais na kuomba aruhusiwe kuishi kijijini kwao.Rais mteule kakataa hilo ombi na kusema lazima ajibu Tuhuma za Makosa yote aliyowatendea Wagambia.

My Note.
Kenya imeonyesha mfano mzuri wa kuheshimu Matakwa ya wananchi.
Kuna haja ya mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la sahara kuiga mfano huo.
 
Wanafiki wakubwa hao! Wanaunga mkono ya Gambia lakini hawaitaki ICC! Mkuki kwa Nguruwe?! Huyu demu msomali Amina Mohamed anawania uenyekiti wa AU kwa hiyo anajikomba kwa ajili ya kura za ECOWAS!
 
Magomeni? Kote huko? Loumoumber tu hapa hawawezi kwa sababu wanasumbua mlimani city ya 1/12 wa ma ropes. Si mnajua walifanya nini na Damien Omen?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom