Kenya yafungiwa nje ya mbio za kupokezana vijiti Rio

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
KENYA haitawakilishwa katika Michezo ya Olimpiki 2016 na timu ya kupokezana vijiti almaarufu Relays. Juhudi za Alphas Kishoyian, Boniface Mucheru, Boniface Mweresa na Haron Koech kuwakilisha Kenya katika mita 4x400 katika Olimpiki 2016 itakayofanyika Agosti 5-21 jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ziligonga mwamba.

Walikuwa wanasubiri kwa hamu Kenya itakuwa miongoni mwa timu 16-bora ifikiapo Julai 12, lakini ilikuwa nje ya viwango vya Shirikisho la Riadha la Dunia (IAAF) kufikia tarehe hiyo ya mwisho ya kufuzu. Kenya ilikamata nafasi ya 18, sekunde 0.35 nje ya Venezuela iliyonyakua tiketi ya mwisho na jumla ya muda wa 6:04.24 baada ya mashindano mawili.

Mataifa ya Cuba, Ufaransa, Urusi, Jamhuri ya Dominica, Poland, Colombia, India na Venezuela yalijaza nafasi nane zilizokuwa zimebaki katika mbio za mita 4x400.

Yalijiunga na Marekani, Bahamas, Ubelgiji, Jamaica, Brazil, Muungano wa Britain, Trinidad & Tobago na Botswana yaliyofuzu moja kwa moja baada ya kumaliza Riadha za Dunia za Relays mwaka 2015 ndani ya nane-bora.

Katika Olimpiki ya 2012 jijini London nchini Uingereza, Kishoyian, Mucheru, Vincent Mumo na Mweresa waliwakilisha Kenya. Hawakufanya vizuri. Waliondolewa baada ya Mumo kumtega Ofentse Mogawane akijaribu kutafuta nafasi ya kupita raia huyo wa Afrika Kusini katika raundi ya kwanza. Afrika Kusini ilikata rufaa na ikashinda kuchukua nafasi ya Kenya katika fainali hiyo.

Kenya itawakilishwa na wanariadha 51. Itawakilishwa katika kitengo cha wanaume na washiriki katika mita 200 hadi marathon, matembezi ya kilomita 20 na fani za uwanjani kurusha mkuki na kuruka juu (High Jump). Katika kitengo cha kinadada, itakuwa na wanariadha kutoka mita 400 hadi marathon pamoja na matembezi ya kilomita 20.

TIMU YA RIADHA YA KENYA YA OLIMPIKI 2016:
Wanaume

Mita 200 - Carvin Nkanata, Mike Mokamb
Mita 800 - Alfred Kipketer, Ferguson Rotich, David Rudisha
Mita 1500 - Asbel Kiprop, Elijah Manangoi, Ronald Kwemoi
Mita 5000 - Caleb Mwangangi Ndiku, Isaiah Kiplangat Koech
Mita 10000 - Paul Tanui, Charles Yosei, Geoffrey Kamworor, Bedan Karoki
Marathon - Eliud Kipchoge, Stanley Biwott, Wesley Korir
Mita 3000 kuruka viunzi na maji - Brimin Kipruto, Conseslus Kipruto, Ezekiel Kemboi
Mita 400 kuruka viunzi - Nicholas Bett, Boniface Mucheru, Haron Koech
High Jump - Mathew Sawe
Kurusha mkuki - Julius Yego
Matembezi kilomita 20 - Samuel Gathimba, Simon Wachira

Wanawake
Mita 400 - Maureen Jelagat, Margaret Wambui
Mita 800 - Margaret Wambui, Eunice Sum, Winnie Chebet,
Mita 1500 - Faith Kipyegon, Nancy Chepkwemoi. Viola Lagat
Mita 5000 - Vivian Cheruiyot, Hellen Obiri, Mercy Cherono
Mita 10000 - Vivian Cheruiyot, Betsy Saina, Alice Aprot
Marathon - Jemima Sumgong, Helah Kiprop, Visiline Jepkesho
Kuruka viunzi na maji - Hyvin Kiyeng, Beatrice Chepkoech, Lydia Rotich
Mita 400 kuruka viunzi - Maureen Jelagat
Matembezi kilomita 20 - Grace Wanjiru.
 
Bila shaka walijaribu, bidii wanayo. Watafaulu kwenye vile vitengo vingine.
 
Back
Top Bottom