Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kwa mara nyingine Kenya imetupiga changa la macho. Wametumia uchomaji wa makanisa Zanzibar kama fursa ya kuwashawishi watalii wasiende Zanzibar ili wabaki Kenya. Ikumbukwe kwamba makanisa yamechomwa Zanzibar wakati ambao magaidi wamelipua mabomu Kenya, lakini hili hawakuliona, na wakasingizia ilikuwa ni hitilafu ya umeme, sio mabomu.
Siku zote nimesema Kenya ni nchi ambayo hatupaswi kuwaamini sana, ukizingatia walikuwa chanzo cha kuvunjika Jumuia ya Afrika Mashariki hapo 1978, na wakasherehekea kuvunjika kwa kunywa champagne waziwazi.
Soma hapa chini.
Wizara ya Maliasili na Utalii juzi ililazimika kutoa tamko la kusahihisha habari za upotoshaji ambazo ziliandikwa na vyombo vya habari vya Kenya na kueleza kuwa Zanzibar kumechafuka na kwa maana hiyo siyo salama kutembelewa na watalii. Hatua hii ni ya kusafisha hali ya hewa ambayo imechafuliwa na vyombo hivyo kwa nia ya ama kuwatisha watalii waliokuwa wanapanga kutembelea visiwa hivyo, au ambao tayari walikuwa njiani kuelekea Zanzibar.
Source: IPPmedia
kenya na zanzibar hali moja......
Kote ni hatari kwenda...........
Na nyie tangazeni kuwa Alshabab wako kibao Nairobi wanalipua Migahawa na mahoteli, wala huhitaji kulalama. Ndo biashara ya ushindani hiyo!!!! Unamchafua mwenzio ili anguko lake liwe kubwa!!!!
I don't think you got me right dude. We, Tanzanians are becoming more of Wailers than Entrepreneurs!Ha ha ha kwa hiyo tuanze mambo ya kina Nape, Maige, Lowasa, n.ke ha ha ha tehe tehe mkuu wangu. Hatutafika mbali kiasi kabisa. For instance kwa sector ya utalii foreigners are very much scared na usalama kwa angle zote!