KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

Mimi mtanzania haki ya mungu nakuja kuoa kenya watoto wangu nataka waishi tu kenya.. bongo bado tunasafari ndefu sana ya ki democracy. Nimeumizwa sana na uchaguz wa 2015.
49baca8fe75e69642427ff794034c680.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kutokufuata katiba huoni kuwa kuna vipengele vya demokrasia havikufuatwa? Yaani iwekwe sheria, isifuatwe , halafu bado tu tuseme kuwa ulikuwa huru na haki!!
Mh haya.
La mimi sisemi hivyo.Ninasema ukiwa na watu maelfu wasimamizi wa kura na vituo 41,000 vya kupiga kura lazima kanuni kadhaa za kikatiba zisiende sawa.Yaani perfection haitaweza kutokea pale ata urudie uchaguzi na hapo ndio majaji walikosea.
 
Katika Bara la Afrika hakuna kiongozi yoyote yule anaye chaguliwa kihalali lazima kutatokea wizi wa kura hakuna haki ya Kidemokrasia ya Vyama vingi Barani Afrika bado tupo nyuma sana Kidemokrasia. Haswa kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais.
 
Katika Bara la Afrika hakuna kiongozi yoyote yule anaye chaguliwa kihalali lazima kutatokea wizi wa kura hakuna haki ya Kidemokrasia ya Vyama vingi Barani Afrika bado tupo nyuma sana Kidemokrasia. Haswa kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais.

Mkuu:
Sio katika Bara la Afrika tu, hata Bara la Marekani Kaskazini (USA) rejea chaguzi zilizopita kwa George Bush Jr. na Donald Trump.
Sijui tufikiri labda ni hulka ya ki-binadamu inayo ambatana na udhaifu wa matamanio au labda kuna kichocheo kikubwa zaidi ya hicho.
 
Nimeona tweet za mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa nk wakipongeza maamzi hayo nikasema nikushauri uwatumbue.

Lipi jipya? Kama kufuta ni jambo la kupongeza hivyo mbona hatukuona tweet za kumpongeza Jecha aliyefuta uchaguzi wa Zanzibar? Uzalendo uko wapi?

Wanasema eti mahakama za Kenya ziko huru! Hawakukusikia siku ile unaongea na wahariri Ikulu uliposema sisi hapa kwetu muhimili mmoja UMECHIMBIWA zaidi?

Eti wanashangaa kwamba wakati hapa tumezuia bunge live wenzetu hata mahakama ziko live kwenye TV!
Mbona hawakupongezi wewe kila unapokwenda uko live? Ndiyo! Kupanga ni kuchagua, wakati Kenyatta hajionyeshi live kwenye mambo yake badala yake bunge na mahakama ndo viko live sisi kwetu rais ndiye yuko live kila siku.
Ndiyo! Kwani yeye siyo kiongozi wa muhimiri wa serikali?
 
Habari wana jukwaa,

Napenda kuwashukuru wakenya wote hasa wakiongozwa na jaji mkuu wataifa la kenya, kwa kusimamia misingi ya sheria bila kujari nani ni nani wala kuruhusu kuingiliwa uhuru wa mahakama.

Kwahilo tu mmetusafisha waafrica, sasa angalau tweweza anza kusema africa ni bala linaloanza kujitegemea kifikra bila kuingiliwa na mtu yeyote, asanteni sana kenya, asante jaji mkuu wa kenya

Naami Tanzania tuna chakujifunza hapo

ASANTENI KENYA

kenya naanza kufikiri kuwaweka katika kundi la hawa wenzetu
afrika kusini
nigeria
ghana
 
Just to ask kwa upande wa technicalities za kisheria, if the comprehensive ruling itatoka after 21 days, je hizo 60 days zitaanza kuwa counted from then or zimeshaanza sasa hivi?

Wataalamu wa sheria tusaidieni kidogo
 
Just to ask kwa upande wa technicalities za kisheria, if the comprehensive ruling itatoka after 21 days, je hizo 60 days zitaanza kuwa counted from then or zimeshaanza sasa hivi?

Wataalamu wa sheria tusaidieni kidogo

zimesha anza kuhesabika, hizo 21 zipo ndani ya 60days
 
Nilichojifunza ni kwamba, kumbe sio lazima kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, Katiba nzuri au Uzalendo bali cha muhimu ni uzingatiaji wa uadilifu na miiko ya utendaji (integrity and professional ethics)! Basi!
Tutafakari!
 
Back
Top Bottom